Wednesday, September 17, 2014

MATOKEO YA UEFA CHAMPION LEAGUE



Mechi zilizochezwa usiku wa kuamkia leo za Klabu Bingwa barani ulaya ambapo Manchester City walianza vibaya michuano hiyo baada ya kupata kichapo cha goli moja bila majibu kutoka kwa wenyeji wao Bayern Munich ya Ujerumani.

Goli la Bayern Munich lilifungwa na Jerome Boateng katika dakika 90

Wakati Man City wakiiadhibiwa ugenini na Bayern Munich, wenzao Chelsea wakiwa nyumbani Stamfode Bridge walitoka na sare ya goli moja kwa moja na Schalke 04.

Bacelona wao waliamua kuushikisha adabu Apoel ya Syprus kwa kuifunga goli moja bila majibu wakati FC Porto ya Ureno wakifungulia mvua ya magoli iliyoambatana radi pale ilipowanyeshea wapinzani wao Bate Borisov ya Belarus kwa jumla ya magoli 6 bila majibu.

Matokeo mengine NK Maribor ya Slovenia ilitoka sare ya 1 - 1 na Sporting Lisbon ya Ureno huku Athletic Bilbao ya Hispania zikitoka uwanjani bila kufungana na Shaktar Donetsk ya Ukraine.

AC Roma ya Italia wao waliiadhibu CSKA Moscow ya Urusi kwa jumla ya magoli 5 -1 huku Ajax na Paris St. Gamaine ya Ufaransa zikitoka sare ya moja kwa moja.

Monday, September 8, 2014

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WAZINDUA MIKOPO YA ELIMU KWA WANACHAMA WAKE

Uzinduzi wa Piga kitabu na LAPF ulikua wa staili ya aina yake kama unavyoonekana katika picha
 Waziri wa Nchi ofisi ya waziri Mkuu Tamisemi Mh. Hawa Ghasia akikabidhi mfano hundi kwa Bwana Rolland Lyamula ambaye ni mwanachama wa LAPF ambaye amenufaika na mkopo wa Elimu

Tuesday, August 26, 2014

Tuesday, August 5, 2014

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA MAREKANI JOHN KERRY ASISITIZA MAZUNGUMZO KATI YA ISRAEL NA PALESTINA




Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry amezitaka pande mbili zinazopingana Israel na Palestina kutia maanani usitishwaji wa mapigano huko ukanda wa Gaza na kuketi katika meza ya mazungumzo.

Bwana Kerry ameiambia BBC kuwaa ni lazima kutia maanani katika pande hizo mbili kuridhiana na kusema kwamba Israel inayo haki ya kujitetea na kujilinda dhidi ya mashambulizi ya maroketi yanayorushwa na Palestina na kukilaumu kikundi cha Hamas kwa mashambulizi hayo lakini pia ametambua kile alichokiita uharibifu mkuwa wa mali na maisha ya watu.

Maelfu ya wapalestina waliokua katika ukanda wa Gaza wamerejeshwa makwao chini ya uangalizi wa umoja wa mataifa katika siku ya kwanza ndani ya saa sabini na mbili za makubaliano ya usitishwaji mapigano baina ya vikundi vya askari wa Israel na Palestina.

Israel imetuma ujumbe huko Cairo ,Misri kujadili juu ya Palestina kusitisha mapigano kwa kipindi kirefu.

Wednesday, July 2, 2014

NDEGE YAUWA WATU WANNE NCHINI KENYA







Watu wanne wameuwawa Jumatano asubuhi baada ya ndege ya mzigo kuanguka katika mtaa wa Utawala mjini Nairobi, na kuharibu majengo mawili kabla ya kuwaka moto.

Walinzi wawili walokua karibu na majengo hayo ya biashara walijeruhiwa, na kutibiwa hospitali. Mkuu wa polisi wa County ya Nairobi Benson Kibue amesema ajali hiyo ilitokea saa kumi alfajiri wakati ndege ya shirika la Skyward kuanguka na kuwaka moto.

Watu wann walokua ndani ya ndege akiwemo rubani ndio waliuliwa, muda mfupi baada ya ndege hiyo kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenyatta mjini Nairobi ikiwa inasafirisha mizigo wa mairungi kuelekea Mogadishu, Somalia.

Sunday, June 29, 2014

MSHAMBULIZI WA UHOLANZI ARJEN ROBBEN AMEKIRI KUJIANGUSHA




Mshambulizi wa Uholanzi Arjen Robben amekiri kuwa alidanganya timu yake ikapewa penalti ya ushindi lakini akasema alikuwa ametegwa.

Kocha wa Mexico Miguel Herrera amemkashifu refarii wa mechi yao na Uholanzi Pedro Proenca kwa kuipendelea Uholanzi .

Herrera amesema kuwa Penalti hiyo dakika tatu kabla ya kukamilika kwa mechi hiyo haikufaa''hiyo ni njama ya FIFA kuiondoa Mexico kwenye kinyang'anyiro hicho.

Robben alianguka katika eneo la hatari la Mexico wakati Uholanzi ilipokuwa imesawazisha bao moja kwa moja na ikaisaidia Uholanzi kuibuka mshindi kwa mabao 2-1.

Penalti hiyo ilifungwa na Jan-Klaas Huntelaar