Mwanamuziki wa kizazi kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C jana amemtembelea Raisi Dkt. Jakaya M. Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu alipokua mgonjwa.
Ray C aliyefuatana na mama yake mzazi Margareth Mtweve na dada yake Sarah Mtweve alimweleza rais kuwa afya yake imeimarika na muda si mrefu atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake. Mama yake pia amemshukuru raisi kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwa ajili ya mwanaye waache kwani matibabu ya ray c yamegharamiwa na raisi.
No comments:
Post a Comment