DODOSO KUHUSU UPATIKANAJI WA NYUMBA BORA KWA WATUMISHI WA UMMA
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ina washukuru watumishi wote waliopata nafasi ya kujaza Dodoso hili. Kama ilivyoelezwa kwenye tovuti awali madhumuni ya dodoso ilikuwa kuiwezesha Kamati ya Mradi wa Ujenzi wa nyumba bora kwa watumishi wa umma kupata taarifa kuhusu mahitaji ya nyumba kwa watumishi. Taarifa hiyo itasaidia kukamilisha mpango wa ujenzi wa nyumba hizo ambao unatarajiwa kuanza mwanzoni mwaka 2013.
Baada ya nyumba hizo kujengwa watumishi wote watafahamishwa kuhusu taratibu za mikopo, aina ya nyumba, mahali zilipo na gharama za nyumba husika. Hivyo tunaombwa kuwa nasubira hadi ujenzi wa nyumba hizo utakapo kamilika.
Inasisitizwa kuwa, dodoso hilo lilihusu taarifa ya mahitaji tu, hivyo kwa wale waliokosa nafasi yakujaza haimaanishi kuwa watakosa fursa ya kukopa baada ya ujenzi wa nyumba utakapokamilika.
Imetolewa na: PRESIDENT OFFICE PUBLIC SERVICE MANAGEMENT http://www.utumishi.go.tz/
0 Comment to "NYUMBA BORA "
Post a Comment