TAARIFA YA
MATOKEO YA MITIHANI YA MAARIFA (QT) NA KIDATO CHA NNE (CSEE)
ILIYOFANYIKA
OKTOBA 2012
1.0
UTANGULIZI
Mitihani ya
Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) kwa mwaka 2012 ilifanyika nchini
kote kuanzia tarehe 8-25 Oktoba 2012. Napenda
kuchukua nafasi hii kutangaza rasmi matokeo ya mitihani hiyo kama
ifuatavyo :
2.0
MTIHANI WA
MAARIFA (QT)
2.1
Usajili na
Mahudhurio
Katika Mtihani wa
Maarifa 2012 watahiniwa waliosajiliwa ni 21,310 ambapo wasichana walikuwa
ni 13,134 na wavulana ni 8,176.
Jumla ya watahiniwa 17,137 sawa na asilimia
80.42 ya waliosajiliwa wamefanya Mtihani.
2.2
Matokeo ya Mtihani wa Maarifa
(QT)
Watahiniwa 5,984 kati ya
17,137 waliofanya mtihani wamefaulu Mtihani
wa Maarifa (QT).
3.0
MTIHANI WA
KIDATO CHA NNE (CSEE) 2012
Jumla ya vituo
5,058 vilitumika katika kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 ambapo
vituo 4,155 vilikuwa vya watahiniwa wa shule na vituo 903 vilikuwa
ni vya watahiniwa wa kujitegemea.
3.1
Usajili na
Mahudhurio ya Watahiniwa
(a)
Watahiniwa
Wote
Jumla ya
watahiniwa 480,036 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012
wakiwemo wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.33 na wavulana
262,453 sawa na asilimia 54.67.
Watahiniwa waliofanya mtihani wa Kidato cha Nne 2012 ni
456,137 sawa na asilimia 95.44. Watahiniwa 21,820
sawa na asilimia 4.55 ya watahiniwa wote waliosajiliwa hawakufanya
mtihani.
(b)
Watahiniwa wa
Shule
Watahiniwa wa
shule waliosajiliwa ni 411,230 wakiwemo wasichana 182,978 sawa na
asilimia 44.50 na wavulana 228,252 sawa na asilimia
55.50. Watahiniwa wa shule waliofanya mtihani
walikuwa 397,136 sawa na asilimia 96.57. Aidha, watahiniwa
14,090 sawa na asilimia 3.43 hawakufanya mtihani kutokana na
sababu mbalimbali zikiwemo utoro, ugonjwa na
vifo.
(c)
Watahiniwa wa
Kujitegemea
Watahiniwa wa
kujitegemea waliosajiliwa walikuwa ni 68,806 wakiwemo wasichana 34,605
sawa na asilimia 50.29 na wavulana 34,201 sawa na asilimia
49.71. Watahiniwa 61,001 wakiwemo wasichana 30,917
na wavulana 30,084 wamefanya
mtihani wakati watahiniwa 7,730 sawa na asilimia 11.23
hawakufanya mtihani.
4.0
MATOKEO YA MTIHANI WA
KIDATO CHA NNE
(a)
Watahiniwa wa Shule
Jumla ya watahiniwa wa shule 126,847 kati ya
watahiniwa 397,136 waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012
wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 46,161 na wavulana ni
80,686.
(b)
Watahiniwa wa Kujitegemea
Idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani
ni 16,112 kati ya watahiniwa 61,001 waliofanya
mtihani. Wasichana waliofaulu ni 6,751 na wavulana ni
9,361.
5.0
UBORA WA UFAULU KWA
MADARAJA NA JINSI
Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata
watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 23,520
wamefaulu katika madaraja I – III ambapo kati yao wasichana ni
7,178 na wavulana ni 16,342.
Mchanganuo wa ufaulu kwa kila Daraja kwa jinsi kwa
Watahiniwa wa Shule mwaka 2012 ni kama ifuatavyo:
Idadi ya
Wavulana
|
Idadi ya
Wasichana
|
Jumla
| |
I
|
1,073
|
568
|
1,641
|
II
|
4,456
|
1,997
|
6,453
|
III
|
10,813
|
4,613
|
15,426
|
I-III
|
16,342
|
7,178
|
23,520
|
IV
|
64,344
|
38,983
|
103,327
|
0
|
120,664
|
120,239
|
240,903
|
6.0
SHULE ISHIRINI
ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE WATAHINIWA 40 AU
ZAIDI
Ubora wa ufaulu wa shule
umepangwa kwa kutumia kigezo cha “Grade Point Average” (GPA)
kuanzia A = 1 hadi F = 5. Shule zenye watahiniwa 40 na zaidi ziko 3,391. Shule
ya kwanza hadi ya ishirini zimeainishwa kwenye Jedwali
lifuatalo :
NAFASI
|
JINA LA SHULE
|
IDADI YA WATAHINIWA
|
MKOA
|
1
|
ST. FRANCIS
GIRLS
|
90
|
MBEYA
|
2
|
MARIAN BOYS
S.S
|
75
|
PWANI
|
3
|
FEZA BOYS
S.S
|
69
|
DAR ES
SALAAM
|
4
|
MARIAN GIRLS
S.S
|
88
|
PWANI
|
5
|
ROSMINI S
S
|
78
|
TANGA
|
6
|
CANOSSA
S.S
|
66
|
DAR ES
SALAAM
|
7
|
JUDE MOSHONO S
S
|
51
|
ARUSHA
|
8
|
ST. MARY’S
MAZINDE JUU
|
83
|
TANGA
|
9
|
ANWARITE GIRLS S S
|
49
|
KILIMANJARO
|
10
|
KIFUNGILO
GIRLS S S
|
86
|
TANGA
|
11
|
FEZA
GIRLS
|
49
|
DAR ES
SALAAM
|
12
|
KANDOTO SAYANSI GIRLS
SS
|
124
|
KILIMANJARO
|
13
|
DON BOSCO SEMINARY
SS
|
43
|
IRINGA
|
14
|
ST.JOSEPH
MILLENIUM
|
133
|
DAR ES
SALAAM
|
15
|
ST.JOSEPH’S ITERAMBOGO
SS
|
64
|
KIGOMA
|
16
|
ST.JAMES SEMINARY
SS
|
44
|
KILIMANJARO
|
17
|
MZUMBE
SS
|
104
|
MOROGORO
|
18
|
KIBAHA
SS
|
108
|
PWANI
|
19
|
NYEGEZI SEMINARY
SS
|
68
|
MWANZA
|
20
|
TENGERU BOYS
SS
|
76
|
ARUSHA
|
7.0
SHULE KUMI AMBAZO
HAZIKUFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE WATAHINIWA 40 AU
ZAIDI
NAFASI
|
JINA LA SHULE
|
IDADI YA WATAHINIWA
|
MKOA
|
1
|
MIBUYUNI
S.S
|
40
|
LINDI
|
2
|
NDAME
S.S
|
41
|
UNGUJA
|
3
|
MAMNDIMKONGO
S.S
|
63
|
PWANI
|
4
|
CHITEKETE
S.S
|
57
|
MTWARA
|
5
|
MAENDELEO
S.S
|
103
|
DAR ES
SALAAM
|
6
|
KWAMNDOLWA
S.S
|
89
|
TANGA
|
7
|
UNGULU
S.S
|
62
|
MOROGORO
|
8
|
KIKALE
S.S
|
60
|
PWANI
|
9
|
NKUMBA
S.S
|
152
|
TANGA
|
10
|
TONGONI
S.S
|
56
|
TANGA
|
8.0
TATHMINI YA UFAULU WA
WATAHINIWA WA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012
8.1
Tathmini ya awali
iliyofanyika kuhusu ufaulu wa watahiniwa katika shule mbalimbali inaonesha kuwa
shule zilizofanya vizuri zaidi ni zile ambazo zina mahitaji yote ya msingi
ikiwemo walimu wa kutosha, miundombinu na vifaa vya kufundishia na
kujifunzia. Aidha, shule zenye ufaulu wa chini ni zile ambazo zina
changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na:
(i)
Baadhi ya shule za vijijini
hazina kabisa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati na pia zina upungufu
mkubwa wa walimu wa masomo mengine;
(ii)
Kutokuwepo kwa maabara kwa shule
zenye mikondo ya sayansi na pia kutokuwepo kwa maktaba kwa ajili ya kujisomea;
na
(iii)
Upungufu mkubwa wa vitabu vya
kiada na ziada. Katika baadhi ya shule uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi ni
1:10.
8.2
Mkakati wa Serikali ni kuendelea
kupunguza changamoto hizo kila mwaka ikiwa ni pamoja na kufanya mambo
yafuatayo:
(i)
Kuajiri walimu kila mwaka ili
kuondoa upungufu uliopo katika shule zetu. Mwaka 2011/2012 Serikali
iliajiri walimu wa sekodari 13,246 na mwaka huu wa fedha 2012/2013
imeajiri walimu 12,973 ambao wamepangwa katika shule zenye
upungufu mkubwa wa walimu. Ajira ya walimu wapya mwaka huu umetuwezesha kuwa na
wastani wa walimu 2-3 kwa shule. Hali hii itaendelea
kuboreka kadri tunavyoendela kuajiri walimu.
(ii)
Kuboresha miundombinu iliyoko
katika shule zetu ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba za walimu, madarasa na
maabara. Mwaka 2012/2013 Serikali imepanga kuboresha miundombinu katika
shule 264 zilizopo katika mazingira magumu ikiwemo miundombinu ya maabara
na nyumba za walimu.
(iii)
Kuendelea kutoa ruzuku ya Tsh
25,000 kwa mwanafunzi kwa mwaka, ambapo asilimia 50 ya fedha hizo ni
kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili kuziwezesha
shule kununua vitabu pamoja na vifaa vingine muhimu kitaaluma.
(iv)
Wizara kuendelea kuzishauri
Halmashauri kuweka mgawanyo mzuri wa walimu waliopo baina ya shule na shule.
(v)
Wizara itaendelea kuimarisha
Idara ya Ukaguzi wa Shule pamoja na kuwawezesha Waratibu Elimu Kata na Wakuu wa
Shule kufanya ukaguzi wa ndani katika Shule za Sekondari zilizo katika maeneo
yao.
9.0
MATOKEO YA MITIHANI
YALIYOZUIWA
Baraza la Mitihani la Tanzania limezuia kutoa
matokeo ya:
(a)
Watahiniwa 28,582 wa Shule ambao hawajalipa ada ya
Mtihani hadi watakapolipa ada wanayodaiwa pamoja na faini; na ikiwa hawatalipa
katika kipindi cha miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa,
matokeo yao yatafutwa.
(b)
Watahiniwa 65 wa kujitegemea na 71 waliofanya
Mtihani wa Maarifa (QT) mwaka 2012 bila ya kulipa ada ya Mtihani hadi
watakapolipa ada pamoja na faini. Ikiwa hawatalipa ada hiyo katika kipindi cha
miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao
yatafutwa.
10.0
MATOKEO YA
MITIHANI YALIYOFUTWA
10.1
Matokeo
Yaliyofutwa Kwa Sababu ya Udanganyifu
Jumla ya watahiniwa 789 wamefutiwa matokeo yao
yote ya mtihani kwa mujibu wa kifungu Na.52(b) cha Kanuni za Mitihani
baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu katika mitihani ya Oktoba
2012. Kati yao, watahiniwa wa shule ni 624 na watahiniwa wa
kujitegema ni 148 na watahiniwa wa Mtihani wa Maarifa (QT) ni 17.
Aina ya udanganyifu uliobainika na idadi ya watahiniwa
husika ni kama ifuatavyo:
S/N
|
AINA YA UDANGANYIFU
|
IDADI YA
WATAHINIWA
|
(i)
|
Watahiniwa kubainika kuwa na skripti zenye miandiko
tofauti au kuwa na miandiko tofauti katika skripti ya somo moja au zaidi ya
moja.
|
04
|
(ii)
|
Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi ndani ya chumba cha
mtihani wakiwa na ‘notes.’
|
170
|
(iii)
|
Watahiniwa kubainika kuwa na mfanano usio wa kawaida wa
majibu.
|
590
|
(iv)
|
Watu kukamatwa wakiwafanyia watahiniwa wengine mtihani
‘impersonation”.
|
04
|
(v)
|
Watahiniwa kukamatwa na simu ndani ya chumba cha
mtihani.
|
06
|
(vi)
|
Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi wakibadilisha
karatasi za maswali au skripti kwa lengo la kufanya
udanganyifu.
|
15
|
|
JUMLA
|
789
|
10.2
Matokeo
Yaliyofutwa Kwa Sababu ya Watahiniwa Kuandika Matusi Katika Skripti
Zao
(i)
Jumla ya watahiniwa 24 waliandika matusi kwenye skripti zao
za masomo mbalimbali. Kitendo hicho ni kosa kwa mujibu wa kifungu 5(13)
cha Kanuni za Mitihani kinachosomeka:
“Written responses to any examination question which
carry words, drawings or pictures connected to sex or abusive language in such a
way that it becomes offensive shall consitute an examination offence and a
candidate who commits such an offence shall be punished by the
Council.”
Kutokana na kosa hilo Baraza la Mitihani limefuta
matokeo yao yote kwa mujibu wa Kifungu cha 6(2)(a)
cha Kanuni za Mitihani kinachosomeka:
“A candidate found to have committed an examination
offence shall - (a) have his examination results
nullified”
(ii)
Kitendo cha kuandika matusi kwenye karatasi za majibu (skripti)
kinaonesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu. Serikali haitaweza kuwavumilia hata
kidogo watahiniwa wa aina hiyo. Hivyo, Serikali itaangalia hatua zaidi za
kisheria za kuchukua dhidi ya watahiniwa wote walioandika matusi.
Kwa mujibu wa kifungu Na. 6(2)(b) cha Kanuni za
Mitihani, watahiniwa wote waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani au
kuandika matusi katika skripti zao hawataruhusiwa kufanya mitihani inayoendeshwa
na Baraza la Mitihani la Tanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja
(01) kuanzia tarehe ya kutangazwa kwa matokeo.
11.0
KUANGALIA MATOKEO YA MTIHANI WA CSEE na QT,
2012
(a)
Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT),
2012 yanapatikana katika tovuti zifuatazo:
·
www.udsm.edu.ac.tz, au
·
www.moe.go.tz
(b)
Matokeo yanaweza
kupatikana pia kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda
namba 15311. Jinsi ya kutuma ujumbe andika:
MATOKEOXNAMBA
YA KITUOXNAMBA YA MTAHINIWA
(Mfano :
matokeoxS0101x0503)
Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa (Mb)
WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA
UFUNDI
0 Comment to "MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 YAMETOKA"
Post a Comment