Maghala ya kuhifadhia bidhaa mbali mbali za wafanyabiashara wa Mwanjelwa, Mbeya yameteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo maghala hayo yapo maeneo ya uwanja wa ndege wa Mwanjelwa
Wanausalama wakiwa makini na vibaka ambao walitaka kuvamia eneo hilo la moto kutaka kupora mali.
Kikosi cha zimamoto cha jiji la mbeya wakishirikiana na kikosi cha zimamoto uwanja wa ndege wa songwe walijitahidi kuuzima moto huo ingawa mara kwa mara waliishiwa maji kutokana na uwezo mdogo wa magari hayo kubeba maji ya kuzimia moto
Maeneo haya kwa kawaida wahalifu hawakosekani.
Polisi wakiwa wamemshika kibaka aliyetaka kuiba mafuta ya kupikia
Gari hili lilipasuka kioo kutokana na vurugu zilizokua zikisababishwa na vibaka pamoja na kurusha mawe
Haya ni mafuta ya kula yaliyomwagika baada ya ndoo za mafuta hayo kuyeyuka kwa moto
Mafuta ya kula
Baadhi ya wafanyabiashara wakijaribu kuangalia baadhi ya bidhaa zao
Muonekano wa maghara hayo baada ya kuzimika kwa moto
Moja ya gari ambalo liliungua na moto huo