Sunday, December 1, 2013

KOCHA MPYA WA AZAM FC AWASILI NCHINI


kocha Joseph Marius Omog raia wa Cameroon akipeana mkono na na Mwenyekiti wa timu hiyo Ndugu Said Mohammed

Omog akionyesha jezi aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa Azam FC


Kocha mpya wa klabu ya Azam FC ameingia nchini, klabu ya Azam inapenda kuufahamisha umma kuwa imeingia mkataba na kocha Joseph Marius Omog raia wa Cameroon kwa kipindi cha miaka miwili (2) kuanzia jana.

Azam Football Club inamuona kocha Omog kuwa anakidhi vigezo vya kuendana na dira ya klabu ambayo ni kukuza na kuwaendeleza wachezaji na kushindana kwa kiwango cha juu kwa lengo la kuwa mabingwa katika mashindano mabalimbali ambayo timu inashiriki.

Uongozi wa Azam FC utampatia ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha malengo na mipango thabiti ya klabu.