Tuesday, April 30, 2013

Willem-Alexander sworn in as king of the Netherlands


Willem-Alexander has been sworn in as king of the Netherlands following the abdication of Queen Beatrix.

He became the country's first king since 1890 when his 75-year-old mother signed the abdication deed earlier on Tuesday after 33 years on the throne.

Huge crowds of orange-clad partygoers are in Amsterdam to pay tribute.

Now known as Princess Beatrix, the former queen maintained a recent Dutch tradition of monarch's handing over power to a new generation.

Wearing the royal mantle, the new king swore to uphold the constitution at a colourful enthronement ceremony in the Nieuwe Kerk, a decommissioned church, before a joint session of the Dutch parliament.

"I swear that I shall defend and preserve the independence and territory of the state with all my powers," he said.

"That I shall protect the general and individual freedom and rights of all my subjects and shall use all available means granted to me by law for preserving and promoting general and individual prosperity as I befitting of a good king.... So help me God almighty."

Crowds in the square outside cheered as the announcement of his inauguration was made from a balcony overlooking the square amid trumpet fanfare.

In the evening, the royal family will take part in a water pageant.

'Happy and grateful'
The queen had announced her intention to stand down in January, saying her son was ready to reign and that it was time for the throne to be held by "a new generation".

She formally relinquished the throne at a short ceremony in the Royal Palace on Tuesday, signing a statement transferring the monarchy to her son "in accordance with the statutes and the constitution of the Kingdom of the Netherlands".

There were huge cheers from the crowds outside in Dam Square, who were watching the ceremony on giant television screens, as she, her son and his wife Maxima - a 41-year-old Argentine-born investment banker - signed the deed of abdication.

Shortly afterwards, the three royals emerged on a balcony above the square.

The visibly emotional Princess Beatrix told the crowds: "I am happy and grateful to introduce to you your new king, Willem-Alexander."

King Willem-Alexander thanked mother for "33 moving and interesting years", saying he and the public and people in Dutch overseas territories were "intensely grateful" to her.

Sunday, April 28, 2013

TUNDU LISSU AHOJIWA NA RADIO TEHRAN KUHUSU SAKATA LA KUKAMATWA MBUNGE LEMA


Nchini Tanzania sakata la kukamatwa na kuwekwa mahabusu Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), kwa madai ya uchochezi, limeibua sura mpya baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutajwa kuwa nyuma ya mkakati huo.

Kwa upande wake Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)kimelaani hatua hiyo na kulilaumu jeshi la polisi mkoani Arusha kwa kukandamiza upinzani.

Chama hicho kimekwenda mbali zaidi na kulituhumu jeshi la polisi Arusha kwamba, limekuwa likitumikia CCM badala ya kutumikia umma.


Viongozi waandamizi wa CHADEMA wamesema, kutiwa mbaroni Godbless Lema ni mkakati wa CCM wa kukabiliana na nguvu ya chama hicho kikuu cha upinzani ambayo imeteka jimbo la Arusha mjini.

 Salum Bendera amezungumza na Bw. Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye anaanza kuelezea jinsi chama chao kilivyopokea hatua ya kutiwa mbaroni Mbunge Godbless Lema.



ARSENAL YAIBANA MAN UNITED EMIRATES



Ligi kuu soka nchini Uingereza imeendelea kwa michezo mitatu iliyopigwa kwenye viwanja vitatu tofauti jijini London jumapili hii.

Manchester United ambao ni mabingwa wa ligi hiyo msimu huu, Hii leo walikuwa wageni wa Arsenal kwenye uwanja wa Emirates Kaskazini mwa london,

Theo Walcot alianza kuifungia Arsenal bao la mapema kabisa dakika ya pili ya mchezo huo ambao BBC ulimwengu wa soka ilikuwa ikuutangaza moja kwa moja.

United walio chini ya Sir Alex Ferguson walionekana kutokuwa kwenye kiwango chao kama mabingwa baada ya kuanza mchezo huo kwa kufanya makosa mengi, na kujikuta wakipewa kadi nne za njano ndani ya dakika 30 za mchezo huo.

Lakini makosa ya safu ya ulinzi wa Arsenal, hasa lile la beki Bakar Sagna la kurudisha mpira kwa kipa wake yaani back pass yaliifanya United isawazishe bao lao kwa njia ya penati baada ya Sagna kutaka kufuta makosa kwa kumchezea vibaya Robin Van Persie ambaye aliifunga timu yake ya zamani bila ya kushangilia.

Dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo kugawana pointi na Arsenal kufikisha pointi 64 pointi mbili zaidi ya wapinzani wao Tottenham ambao walitoka sare pia hapo jana na Wigan.

Kwingineko Mashariki mwa jiji la London kulikuwa na michezo miwili kwenye viwanja tofauti,

Chelsea wakiwa wenyeji wa Swansea kwenye uwanja wa Stamford Bridge, Mchezo uliomalizika kwa vijana wa Roman Abromavich kuibuka na ushindi wa 2-0, Mabao yao yakifungwa na Mbrazil Oscar Dos Santos Junior huku Frank Lampard akifunga kwa mkwaju wa penati.

Na Mchezo wa awali kabisa ulichezwa kwenye uwanja wa Roftus Road kwa QPR kupambana na Wigan, Mchezo ambao ulimalizika kwa sare bila kufungana.

Matokeo hayo ya sare kwa QPR na Wigan yalizifanya timu zote mbili kushuka daraja la ligi kuu.

Mechi nyingine itapigwa hapo kesho kati ya Aston Villa na Sunderland, Mechi ambayo itakuwa ni ya kukata na shoka kwani timu zote mbili zinajitutumua kutoshuka daraja

Sunday, April 21, 2013

LUIS SUAREZ AMEOMBA RADHI KWA KUMNG'ATA BRANISLAV IVANOVIC

Ivanovic akimuonyesha mwamuzi alivyong`atwa

Branislav Ivanovic na Luis Suarez

Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez ameomba radhi kutokana na kitendo chake cha kumng'ata mkononi beki wa Chelsea Branislav Ivanovic wakati timu hizo mbili zilipocheza jumapili jioni kwenye mchezo wa ligi kuu soka nchini Uingereza.

Suarez,amesema binafsi anasikitishwa na kitendo alichokifanya na amempigia simu Ivanovic na kumuomba radhi yeye mwenyewe kwani anajutia kitendo alichomfanyia,na kushuruku kwa kuwa Ivanovic amemsamehe.

Kitendo hicho kilitokea katika kipindi cha pili cha mechi baina ya Liverpool na Chelsea,Mechi iliyoishia kwa sare ya 2-2 huku Suarez akifunga bao la dakika za mwisho la kuisawazishia Liverpool. Ivanovic alimuonyesha mwamuzi Kevin Friend sehemu aliyong'atwa na Suarez lakini mwamuzi alionekana kutotilia maanani kwa kuwa hakukiona kitendo hicho.

Wachambuzi wa masuala ya kandanda nchini Uingereza wamekitaja kitendo hicho cha Suarez kama tukio lisilokubalika katika mchezo wa soka,huku wakisema huenda akakabiliwa na adhabu kali kutoka chama cha soka nchini Uingereza FA.

Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema ameangalia video ya tukio hilo mara baada ya mchezo na amesikitishwa na kitendo hicho na kumueleza Suarez kuwa kitendo hicho hakikubaliki michezoni,huku akisisitza kuwa hakuna mchezaji ambaye ni mkubwa zaidi ya klabu hiyo. Naye Mkurugenzi wa klabu hiyo ya Liverpool Ian Ayre amesema kitendo alichokifanya Suarez hakistahili kufanywa na mchezaji wa klabu hiyo.

Liverpool imesema itatoa adhabu stahili kwa kitendo hicho wakati wakisubiri adhabu yoyote kutoka chama cha soka cha Uingereza FA.

Suarez sio wa kwanza kufanya kitendo cha kumng'ata mchezaji uwanjani kwenye ligi kuu ya Uingereza,kwani mwaka 2006, mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Jermain Defoe alimng'ata kiungo wa West Ham wa wakati huo Javier Mascherano katika mchezo wa ligi kuu kwenye uwanja wa White Hart Lane.

Defoe alifanya kitendo hicho baada ya kuchukizwa na rafu aliyochezewa na Mascherano ambapo mwamuzi Steve Bennett aliwazawadia kadi za manjano wote wawili na baadaye chama cha soka cha Uingereza FA kilisema hakitoa adhabu yoyote kwa kuwa mwamuzi alikiona kitendo hicho na kuwaadhibu uwanjani.