Padre E. Mushi Paroko wa parokia ya Minara Miwili Zanzibar ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika.
Hii ni gari aliyokuwamo Padri Mushi.
Paroko huyu amepigwa
risasi akishuka katika gari lake wakati akienda kuendesha ibada ya saa 3.00
jana.
Padri Evarist Mushi
amepigwa risasi kichwani na kufa papohapo na watu wasiojulikana akiwa njiani
anaenda kuendesha misa katika Kanisa la Mt.Theresia eneo la Mtoni
Zanzibar.
Msemaji wa Jeshi
Polisi Zanzibar Inspekta Mohamed Mhina amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
amesema kuwa padre huyo ameuawa wakati akijiandaa kuingia kanisani akitokea
kwenye gari yake ambapo ndipo alipofikwa na umauti
huo.
Jeshi la Polisi visiwani humo kupitia kwa Msemaji wake Mkaguzi wa Polisi, Mohamed Mhina limelaani mauaji hayo na na kusisitiza kuwa Jeshi limeanza msako mkali wa kuwabaini wauaji hao.
Hili ni tukio la pili
kutokea Zanzibar ambapo tukio la kwanza lilitokea kwa Padre Ambrose Mkenda
kupigwa risasi na kujeruhiwa na watu wasiojulikana.
0 Comment to "MAUAJI YA PADRI MUSHI ZANZIBAR"
Post a Comment