Thursday, November 1, 2012

FAIDA YA KITUNGUU MAJI

UKIJUA FAIDA YA KITUNGUU MAJI HUTAACHA KUKITUMIA
Baadhi ya magonjwa ambayo hadi sasa haijafahamika tiba yake katika hospitali zetu yanayotibika kwa kitunguu maji ni pamoja na saratani (Cancer), kisukari, vidonda vya tumbo, presha, na pumu. Dawa hii pia ni tiba ya kifua kikuu.
Assalaam alaykum mpenzi msomaji; baada ya juma lililopita kuzungumzia kitunguu swaum kama dawa inayotibu magonjwa mengi ikiwemo Saratani, leo nitazungumzia tiba ya magonjwa mbalimbali kwa kutumia kitunguu maji.
Mbali ya kitunguu maji kutumika kama kiungo katika mboga zetu, lakini pia ni tiba inayotumika sana nchini Misri na imeonesha mafanikio kwa kutibu maradhi mbalimbali, yakiwemo yale yasiyo na tiba katika hospitali nyingi hapa nchini.
Baadhi ya magonjwa ambayo hadi sasa haijafahamika tiba yake katika hospitali zetu yanayotibika kwa kitunguu maji ni pamoja na saratani (Cancer), kisukari, vidonda vya tumbo, presha, na pumu. Dawa hii pia ni tiba ya kifua kikuu.
Kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali wa masuala ya tiba, kitunguu maji kina uwezo wa kufungua hamu ya kula, hutia kiu, hulainisha chakula tumboni na huleta hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume na wanawake.
Aidha mtaalamu mmoja anayefahamika kwa jina la Ibn Baitar amepata kunukuliwa akisema kwamba, kitunguu maji huingiza kwa wingi vitamin C katika mwili wa binadamu ambayo inasaidia sana kuona vizuri.
Lakini pia ndani ya kitunguu maji zimo chembechembe zenye kuua vijidudu (Bacterias) na ndio maana dawa hii ina uwezo pia wa kutibu kifua kikuu (TB), kaswendwe na kisonono.
Hivyo kupitia makala yetu haya, tunawashauri watu wapendelee sana kutumia kitunguu maji kwa ajili ya kinga na tiba ya maradhi katika miili yetu.
Na imethibitika kuwa wagonjwa wengi waliowahi kutumia tiba ya kitunguu maji kwa muda mrefu wamepata nafuu na wengine hupona kabisa maradhi yao.
Sasa ebu tuangalie matumizi sahihi ya dawa ya kitunguu maji;
Kwa mgonjwa wa kifaduro, pumu, vidonda vya tumbo, presha, kifua kikuu, malaria na ugonjwa wa matumbo (typhold) anatakiwa mgonjwa kuchukua juisi ya kitunguu maji ujazo wa kikombe cha kahawa achanganye na asali mbichi ujazo wa nusu lita, kisha aitumie kwa kula katika ujazo wa kijiko kikubwa asubuhi na jioni.
Ama wale wagonjwa wanaosumbuliwa na matatizo ya nguvu za kiume wanashauriwa watafune kitunguu maji kibichi kwa muda wa siku saba asubuhi na jioni.
Na maradhi yote yaliyobakia yanatibika kwa njia mbili zifuatazo;- kwanza kwa njia ya kiungo katika mboga na pili ni kwa kutafuna kitunguu chenyewe kila siku na Mola Muumba akipenda matatizo yatapungua ama kwisha kabisa.
Aidha kwa mgonjwa wa mapunye na kunyonyoka nywele kichwani anaweza kujitibu kwa kukipondaponda vizuri, alafu achanganye na mafuta ya zaituni, kisha apake kichwani mpaka atakapoona tatizo limekwisha.

Share this

0 Comment to "FAIDA YA KITUNGUU MAJI "

Post a Comment