Thursday, May 30, 2013

MATOKEO MAPYA YA KIDATO CHA NNE YATANGAZWA




Baraza la mitihani Tanzania NECTA limetangaza rasmi matokeo ya Kidato cha Nne 2012. Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu.

Matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57.

Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.
 
Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.

Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.

Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.

Tuesday, May 28, 2013

R.I.P. MANGWEA

Magwea amefariki  jana asubuhi alikuwa Ghetto moja Na msanii M To The P.
Walivyokwenda kuwagongea asubuhi walikuta Ngwear amefariki na M To The P amepoteza fahamu kabisa. Pia Daktari alishatoa taarifa kwa watu wa karibu wa Ngwear huko South Africa. Ngwea akiwa na msanii M to the P jana south Africa mtu wa karibu anasema walitakiwa kurudi dar jana lakini waliwakuta wamezima kwenye room wote wawili baada ya kuji overdose madawa ya kulevya na M to the P yupo hoi hospitali.

Monday, May 27, 2013

BANDARI YA DAR ES SALAAM NI KICHOCHEO CHA UCHUMI – BENKI YA DUNIA



Tanzania na mataifa jirani ya Afrika Mashariki yanatajwa kuwa yanaweza kuboresha pato la ndani la mwaka – GDP – kama yatachukua hatua za kuboresha ubora wa bandari ya Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ripoti mpya iliyopewa kichwa cha ‘Opening the Gates: How the port of Dar es Salaam can transform Tanzania’ iliyoandikwa na Jacques Morisset, mchumi mkuu wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Uganda na Burundi, Tanzania na majirani zake wanaweza kuongeza pato lao la ndani kwa kiwango kikubwa.

Ripoti hiyo inasema Tanzania inaweza kuongeza pato lake la ndani kwa kiasi cha dola bilioni 1.8  na nchi jirani zinaweza kupandisha pato la ndani kwa dola milioni 830 kwa mwaka, kiwango ambacho kinaelezewa ni hasara iliyotokea mwaka 2012.

Ripoti hiyo inasema kuwa bandari ya Dar es Salaam iko katika njia kuu ya biashara ya Tanzania kwa asilimia 90, na inashughulikia bidhaa zinazogharimu dola bilioni 15 kwa mwaka, sawa na asilimia 60 ya pato la ndani la Tanzania kwa mwaka 2012.

Bandari hiyo pia inaelezewa kuwa inatumiwa na majirani sita wa Tanzania, ambao nchi zao hazina bandari, nchi hizo ni Malawi, Zambia, Burundi, Rwanda, Uganda na mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Mwaka 2012 pekee, ripoti inasema hasara ya jumla inayoelezewa ambayo imetokea katika bandari hiyo imefikia dola bilioni 1.8 kwa uchumi wa Tanzania na dola milioni 830 kwa nchi jirani. Hasara ambayo ni sawa na asilimia saba ya pato la ndani la mwaka la Tanzania, na kwa kiasi kikubwa imeathiri wanunuzi wa ndani, biashara na mashirika ya serikali.

Moja ya sababu ambazo inaelezewa zimechangia katika hasara hii ni utendaji mbaya wa bandari ya Dar es Salaam ambao umezigharimu nchi nyingine jirani nazo kupata hasara, na hivyo kulazimika kulipa fedha zaidi kwa bidhaa zinazoagiwa kutoka nje, ikiwemo bidhaa za msingi kama vile mafuta ghafi, simenti, mbolea na madawa.

Moja ya vigezo  vilivyoelezewa katika ripoti ambavyo vinachangia katika kusababisha  hasara ni pamoja na uchelewesho unaozikabili meli ambazo zinafika katika bandari ya Dar es Salaam.  Katikati ya mwaka 2012, meli zilisubiri kwa takriban siku 10 ili kuweza kuruhusiwa kutia nagan na siku 10 nyingine za ziada ili kuweza kushusha mizigo.

Rushwa pia imetajwa kuwa ni kigezo kingine kinachochangia katika utendaji mbaya wa Bandar, kama chanzo cha utendaji mbaya na kusababisha hasara kubwa.

RAIS OMAR AL BASHIR ANATISHIA KUFUNGA BOMBA LA MAFUTA



Rais wa Sudan Omar al Bashir anatishia kufunga bomba linalobeba mafuta kutoka Sudan Kusini kwenda kaskazini , anasema kusini inaunga mkono waasi.

Bw.Bashir alisema katika hotuba ya Televisheni Jumatatu kwamba Sudan itafunga bomba hilo  la mafuta, kama Sudan Kusini itawapa uungaji mkono wa aina yeyote waasi, katika  maeneo ya mpakani ya Kordofan Kusini na Blue Nile  na eneo lenye utete mkubwa la magharibi la Darfur.

Rais huyo akilindwa   na maafisa wa jeshi, alizungumza  baada ya jeshi kusema limechukua tena mji wa Abou Kershola kutoka kwa waasi huko Kordofan Kusini.