Tuesday, November 26, 2013

FINANCE AND ADMINISTRATION ASSISTANT – 1 position



REPOA is currently seeking applications from interested individuals for the position of Finance and Administration Assistant.


JOB SUMMARY:

 Reporting to the Senior Accountant, the job holder will provide the Department of Finance and Administration with financial and administrative support.

 Key responsibilities

FINANCE

 a) Process daily payments and ensure that financial transactions are in accordance with REPOA financial rules and regulations

b) Process subsidiary and general ledgers

 c) Provide assistance to ensure proper management of departmental budgets.         

d) Support preparation of final accounts


ADMINISTRATION

 e) Assist in the process of recruitment of staff

f) Assist in updating Human Resource policies and procedures

 g) Provide support in ensuring that Health and Safety Regulations are complied with

 h) Support in coordination of general maintenance and repairs of assets


MINIMUM REQUIREMENTS:

 • A degree in Accountancy/business administration or equivalent qualifications from a recognized Institution.

 • Excellent administrative skills

 • At least one year work experience in accounting department

 • Knowledge of financial systems including PASTEL accounting software

 • Attention to detail and accuracy

 • Excellent communication skills, both written and verbal

 • Ability to work calmly under pressure and keep to deadlines

 • Ability to work independently but also as part of a small team

 • IT literate


MODE OF APPLICATION:

 Qualified applicants are welcome to apply, and should send their typed application letter and detailed CV including three referees to the address below by 3rd December 2013

 
REPOA IS AN EQUAL OPPORTUNITY EMPLOYER.

 Only applicants who meet requirements will be considered for an interview. Those who do not hear from REPOA should consider themselves unsuccessful.

Applications should be addressed to The Executive Director, REPOA

Wednesday, November 13, 2013

ZANZIBAR WAKAMATA MENO YA TEMBO



 
Polisi nchini Tanzania wamekamata vipande elfu moja na ishirini na moja vya meno ya tembo vyenye uzito wa karibu kilo elfu tatu.

Meno hayo ya tembo yamekamatwa katika bandari ya Zanzibar jana na watu wawili wanashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na meno hayo. Hata hivyo, bado haijafahamika idadi kamili ya tembo waliouawa, kwani baadhi ya meno yamekatwa vipande.

Kwa mujibu wa afisa habari mkuu wa jeshi la polisi Zanzibar, Inspekta Mohammed Mhina, kiasi kilichokamatwa ni kikubwa kuwahi kukamatwa visiwani humo. Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, alisema meno hayo yalikuwa yamehifadhiwa katika kontena la futi arobaini yakiwa yamechanganywa katika mifuko iliyohifadhi makombe ya konokono wa baharini, tayari kwa kusafirishwa nje.

Hivi karibuni raia watatu wa China walikamatwa nchini Tanzania kwa kukutwa na meno 706 ya tembo, sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi mbalimbali nchini humo.

Kukamatwa kwa meno haya ya tembo, kumekuja wakati tayari serikali imetangaza kusitisha Operesheni Tokomeza Ujangili, ambayo ililenga kunusuru wanyama walio hatarini kutoweka kutokana na kuuawa katika hifadhi za taifa nchini Tanzania. Wanyama wanaolengwa zaidi na majangili kutokana na meno yao na pembe ni tembo na faru.

Matukio ya kukamatwa kwa meno ya tembo kutoka Afrika Mashariki yamekuwa yakiripotiwa kila mara. Oktoba, 20, 2012, tani nne za meno ya tembo yenye thamani ya dola milioni 3.4 za Kimarekani yalikamatwa Hong Kong, yakidaiwa kusafirishwa kutoka Kenya na Tanzania.

Pia Agosti 16 mwaka huu polisi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, walimkamata raia wa Vietnam akiwa na meno ya tembo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 18 sawa na dola zaidi ya elfu 11, yakisafirishwa kwenda nje.

Friday, November 8, 2013

AZAM FC YAMTIMUA KOCHA


Huku ligi kuu soka Tanzania Bara ikiwa imekamilisha mzunguko wake wa kwanza, timu ya Azam FC ya Dar es Salaam imetangaza kusitisha mkataba na kocha wake mkuu Stewart Hall wa Uingereza kwa kile kilichoelezwa kama makubaliano ya pamoja.
Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa klabu hiyo jijini Dar es Salaam, hii itakuwa ni mara ya pili kwa kocha huyo kuachana na klabu ya Azam na ameafikiana na uongozi wa klabu hiyo baada ya kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo ambapo timu ya Azam sasa inashika nafasi ya Pili baada ya kwenda sare ya mabao 3-3 na timu ya Mbeya City ambapo zote sasa zina Pointi 27. Bingwa mtetezi timu ya Yanga inaongoza ligi hiyo kwa sasa ikiwa na pointi 28 baada ya kuinyuka Oljoro JKT mabao 3-0 katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo, maaruf kama Vodacom Premier League.
Klabu ya Azam FC inayoinukia kwa ubora wa miundo mbinu huku ikiendeshwa kisasa kwa mipango inayoeleweka kinyume na klabu nyingi nchini Tanzania imekuwa ikifanya vema chini ya mwalimu huyo ambapo msimu uliopita aliiwezesha kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kushika nafasi ya Pili katika Ligi kuu msimu uliopita.
Klabu hiyo inao wachezaji kadhaa wa Kulipwa kutoka nchi za Ivory Coast, Kenya na Uganda. Kuachia ngazi kwa kocha huyo kunaelezwa kuwa kumekuwa kwa mkakati ili kusiathiri mwenendo wa timu hususan wakati ligi ikiendelea na sasa kutaiwezesha Azam FC Kutafuta kocha mwingine hususan wakati huu ambapo ligi imefikia Mapumziko.