JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na. EA.7/96/01/C/67 30 Novemba, 2012
KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mbeya Institute of Science and Technology (MIST), Water Development Management Institute (WDMI) na Tea Research Institute of Tanzania (TRIT) anatarajia kuendesha usaili na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi, waombaji kazi watakaofaulu usaili.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anawatangazia waombaji wa fursa za ajira kwa tangazo lililotolewa tarehe 28/05/2012, 29/06/2012 na 27/07/2012 za Mamlaka za Ajira zilizotajwa hapo juu kuwa wamechaguliwa kufanya usaili.
Wasailiwa wanashauriwa kuzingatia yafuatayo:
- UKAGUZI WA VYETI UTAANZA SAA 1:00 HADI 1:30 ASUBUHI SIKU YA MTIHANI WA MCHUJO.
- KUJA NA KITAMBULISHO KWA AJILI YA UTAMBUZI MFANO: KITAMBULISHO CHA MKAZI, KUPIGIA KURA, BENKI, KAZI, HATI YA KUSAFIRIA N.K
- Kuja na Vyeti Halisi (original certificates) za kuanzia kidato cha nne, sita, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji.
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).
- Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
- Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyiwa usaili
- Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
- Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba tena mara nafasi za kazi zitakapotangazwa.
NB: Kwa Maelezo zaidi Tangazo hili linapatikana pia katika tovuti zifuatazo:-