Waziri wa Mambo ya Nje
wa Marekani John Kerry amezitaka pande mbili zinazopingana Israel na Palestina
kutia maanani usitishwaji wa mapigano huko ukanda wa Gaza na kuketi katika meza
ya mazungumzo.
Bwana Kerry ameiambia
BBC kuwaa ni lazima kutia maanani katika pande hizo mbili kuridhiana na kusema
kwamba Israel inayo haki ya kujitetea na kujilinda dhidi ya mashambulizi ya
maroketi yanayorushwa na Palestina na kukilaumu kikundi cha Hamas kwa mashambulizi
hayo lakini pia ametambua kile alichokiita uharibifu mkuwa wa mali na maisha ya
watu.
Maelfu ya wapalestina
waliokua katika ukanda wa Gaza wamerejeshwa makwao chini ya uangalizi wa umoja
wa mataifa katika siku ya kwanza ndani ya saa sabini na mbili za makubaliano ya
usitishwaji mapigano baina ya vikundi vya askari wa Israel na Palestina.
Israel imetuma ujumbe
huko Cairo ,Misri kujadili juu ya Palestina kusitisha mapigano kwa kipindi
kirefu.
0 Comment to "WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA MAREKANI JOHN KERRY ASISITIZA MAZUNGUMZO KATI YA ISRAEL NA PALESTINA"
Post a Comment