Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, amezungumza wazi
kwa mara ya kwanza kuhusu kutekwa kwa waschana takriban 200 wa shule kaskazini
mashariki mwa nchi hiyo.
Katika taarifa yake ya kwanza hadharani tangu
wasichana 200 kutekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Waislamu
wenye itikadi kali wa Boko Haram, Rais Goodluck Jonathan, amesema kuwa kila
juhudi zinapaswa kufanywa kuwakomboa wasichana hao.
Tangazo la Rais lilitolewa kufuatia shinikizo
zilizotolewa na familia, makundi ya wanawake na watu wengine ambao wameitaka
Serikali kufanya bidii zaidi kuhakikisha kuwa wasichana hao wanakombolewa.
Rais alisema kuwa maafisa wa usalama wamekuwa
wakitafuta kila mahali wakitumia ndege na helikopta lakini akakiri kuwa
hawajafaulu kutambua walikofichwa wasichana hao.
Alisema kuwa Serikali yake imelazimika kuomba msaada
katika kuwatafuta wasichana hao kutoka Serikali za Marekani, Uingereza na
Uchina.
Jeshi la Nigeria limekuwa likipambana na kundi hilo
la wapiganaji tangu mwaka 2009, lakini mashambulizi na milipuko ya mabomu
yameendelea kusikika kila mahali bila kukoma.
Hivi majuzi kumekuwa na milipuko katika mji mkuu wa Abuja
katika muda wa majuma matatu ambapo karibu watu 90 waliuawa na wengine wengi
kujeruhiwa.
Mnamo Jumatano Kongamo la Dunia juu ya Uchumi wa
Afrika utafanyika mjini Abuja na swala la usalama limewatia maafisa wa usalama
tumbo joto, ambapo imetangazwa kuwa siku hiyo shule zote na afisi za Serikali
zitafungwa ili kuimarisha usalama eneo hilo la mkutano.
0 Comment to "RAIS WA NIGERIA AHAIDI KUPATIKANA KWA WASICAHANA"
Post a Comment