Wajumbe waliokuwa na
taarifa kuhusu mkutano wa faragha, walisema kuwa mwenyekiti wa kamisheni ya AU
Bi Nkosazana Dlamini Zuma, aliwaambia wajumbe wa baraza la usalama kuwa kesi
dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu rais William Ruto zinapaswa kuahirishwa
kwa mwaka mmoja.
Alitaja shambulizi la
hivi karibuni, katika jengo lenye maduka la Westgate huko mjini Nairobi,
akisema viongozi hao wa Kenya wanahitajika nyumbani ili kushughulikia usalama
wa taifa lao na hawawezi kuwa katika mahakama huko the Hague kwa muda wa wiki
kadhaa kila wakati.
Umoja wa Afrika
umepanga kufanya mkutano maalum wa viongozi hapo kesho na Ijumaa kujadili suala
ICC. Ombi rasmi la kucheleweshwa kwa kesi ya viongozi hao huwenda linaweza
kutolewa baada ya mkutano huo.
Baraza la usalama la
umoja mataifa lina mamlaka ya kutoa kile kinachojulikana kama kipengele cha 16
kinachowezesha kesi kuahirishwa katika mahakama ya ICC. Lakini uwamuzi kama huo
unahitaji makubaliano kutoka kwa wanachama wote 15 wa baraza hilo.
Rais wa Kenya na naibu
wake wameshitakiwa kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 na
2008, na zilizosababisha vifo vya zaidi
ya watu elfu moja na kuwafanya takriban wengine nusu millioni kupoteza makazi
yao.
Nchi 34 barani Africa
ni wanachama wa mahakama ya ICC, lakini hivi karibuni wamekuwa wakiikosoa
mahakama hiyo, wakisema inaushawishi wa kisiasa na inawalenga kwa uonevu,
viongozi wa kiafrika.
Mkuu wa idara ya mradi
wa haki wa kundi la Human Rights watch,
Richard Dicker, anasema ukosoaji wa Mahakama hiyo, unaofanywa na waafrika
haujastahiki.
Kumekuwepo na
mazungumzo ya kutaka kujiondoa kwa nchi nyingi za kiafrika kutoka mahakama
hiyo, lakini pendekezo la Bi. Zuma la kutaka kucheleweshwa kwa kesi kunaashiria
hakuna uungaji mkono mkubwa kwa Kenya ambao wengineo walotarajia ili waweze
kuwa na sauti kubwa.
Katika mkutano wa umoja
wa Afrika na umoja mataifa huko Addiss Ababa, wanadiplomasia walisema kwa
mujibu wa utaratibu, baraza la usalama litatafakari ombi kucheleshwa kwa kesi
iwapo ombi hilo litawasilishwa, lakini kuhusu suala la ICC baraza hilo
limegawika.
Wakati wanachama wa
baraza wanakubaliana kuwa mahakama ni chombo muhimu cha kupigana dhidi ya
watuhumiwa kutohukumiwa, lakini ni wanachama 6 tu kati ya 15 wa baraza hilo la
usalama, waloidhinisha makubaliano ya Rome, yaliyopelekea kuundwa kwa ICC.
Marekani ni miongoni ya wasoidhinisha, lakini utawala wa rais Barack Obama
umeelezea nia yake ya kushirikiana na
chombo hicho.
0 Comment to "MWENYEKITI WA KAMISHENI YA AU APENDEKEZA KESI YA KENYATTA NA RUTTO IHAIRISHWE"
Post a Comment