Kambi ya Wakimbizi Dadaab nchini Kenya
Kamati ya bunge
inayohusika na ulinzi na uhusiano na mataifa ya kigeni imependekeza kufungwa
kwa kambi za wakimbizi nchini Kenya, ikisema zinatishia usalama wa nchi.
Mwenyekiti wa kamati
hiyo Ndungu Githinji amesema kuwa wana habari kuwa kambi zilizoko kwenye mipaka
ya Kenya hutumika kuwapa mafunzo wapiganaji wa kiislamu.
Kenya inahifadhi
wakimbizi wa kisomali zaidi ya nusu milioni katika kambi za Dadaab zilizoko
kwenye mpaka na Somalia.
Mwenyekiti huyo Ndungu
Githinji ameambia BBC kuwa miaka 22 imetosha kwa usaidizi kwa wasomali hao na
wanastahili sasa kurudi nyumbani baada ya amani kurejeshwa nchini mwao.
''Hawa wakimbizi
wamekaa miaka ishirini na mbili Kenya. Ningependa kuuiomba UN ifunge kambi
hizo. Iwarudishe wasomali kwao, maana sasa nao pia wanayo serikali yao. Ili
tuweze kukaa kwa amani.''Amesema bwana Githinji.
Lazima
usalama uimarishwe
Bwana Githinji pia
ametoa wito kwa vyombo vya usalama kuzidisha usalama na doria katika maeneo
yanayotishiwa kushambuliwa na Al shabaab.
''Tunasikia AL shabaab
wanasema kwamba bado wanataka kutupiga. Naomba kuwa zile sehemu zote
walizotoshia kushambulia zipewe ulinzi wa kutosha kwa saa ishirini na nne.''
Wanamgambo wa Alshabaa
wamekuwa wakijihusisha na waislamu katika harakati zao huku wakidai kuwa
wanapigania haki ya dini ya kiislamu nchini Somalia na hata mataifa jirani kama
vile Kenya.
Pia wamekuwa wakilenga
Kenya kwa mashambulio kufuatia hatua ya Kenya kuingia nchini Somalia mwaka wa
2011 kuwaondoa wanamgambo hao kwa madai kuwa wanatishia usalama wa nchi.
Kutokana na hilo
wabunge waliozuru eneo la shambulio kule Westgate wamefurahishwa na hatua ya
waislamu nchini Kenya kujiepusha na kundi hilo la AL-Shabaab.
Mwenyekiti Githinji
asema, '' Ningependa kupongeza viongozi wa waislamu ambao wametoa taarifa yao
kuwa hawaungi mkono mashambulio haya.''
Mwandishi wa BBC jijini
Nairobi anasema kuwa wito huu wa kufungwa kwa kambi za wakimbizi za Dadaab na
Kakuma, zimekuwepo kwa muda. Wakenya wengi wanahisi kuwa Kuwepo kwa wakimbizi
hao kumeendelea kuiweka nchi hiyo katika hatari ya mashambulio. Lakinim bali na
hilo.
Pia baadhi wanahisi
wakimbizi hao ndio wa kulaumiwa kwa kupanda gharama ya makaazi hasa katika
maeneo ya Nairobi kama vile Eastleigh, wanakoishi kwa wingi zaidi.
0 Comment to "WABUNGE NCHINI KENYA WATAKA WAKIMBIZI WAONDOLEWE"
Post a Comment