Mshambulizi
wa Uholanzi Arjen Robben amekiri kuwa alidanganya timu yake ikapewa penalti ya
ushindi lakini akasema alikuwa ametegwa.
Kocha
wa Mexico Miguel Herrera amemkashifu refarii wa mechi yao na Uholanzi Pedro
Proenca kwa kuipendelea Uholanzi .
Herrera
amesema kuwa Penalti hiyo dakika tatu kabla ya kukamilika kwa mechi hiyo
haikufaa''hiyo ni njama ya FIFA kuiondoa Mexico kwenye kinyang'anyiro hicho.
Robben
alianguka katika eneo la hatari la Mexico wakati Uholanzi ilipokuwa
imesawazisha bao moja kwa moja na ikaisaidia Uholanzi kuibuka mshindi kwa mabao
2-1.
Penalti
hiyo ilifungwa na Jan-Klaas Huntelaar
0 Comment to "MSHAMBULIZI WA UHOLANZI ARJEN ROBBEN AMEKIRI KUJIANGUSHA"
Post a Comment