Monday, June 2, 2014

PETER MUTHARIKA ASHINDA UCHAGUZI WA MALAWI

Peter Mutharika akisalimia wananchi



Rais Kikwete akisalimiana na Rais Joyce Banda aliyeondoka madarakani leo baada ya kushindwa uchaguzi na Peter Mutharika huku Kinana akionekana kwa mbali sana.


Kiongozi wa chama cha upinzani cha Democratic Progressive nchini Malawi, Peter Mutharika, ameapishwa leo kama rais wa nchi hiyo. Bw Mutharika mwenye umri wa miaka 74 alisema katika hotuba fupi kuwa kazi yake kubwa itakuwa kuwaunganisha wamalawi baada ya mvutano wa muda mrefu katika maswala ya uchaguzi.

Ametoa wito kwa washindani wake kuungana naye katika kujenga taifa. Maafisa uchaguzi Ijumaa walimtangaza Mutharika kama mshindi wa uchaguzi wa wiki iliyopita uliokuwa na utata na kumshinda rais aliyekuwa madarakani Joyce Banda.

Tume ya uchaguzi ya Malawi ilitangaza matokeo hayo Blantyre, saa kadha baada ya waandamanaji waliokuwa wakidai hesabu mpya ya kura kupambana na polisi katika mji wa Mangochi – kusini mwa nchi. Inaripotiwa kuwa mtu mmoja alifariki katika ghasia hizo.

Hesabu ya mwisho inayonyesha kuwa Bw Muthariki alipata kiasi cha asilimia 36 ya kura, na chama cha Malawi Congress cha Lazrous Chakwera kilipata asilimia 29. Rais Banda alimaliza na asilimia 20 tu ya kura. Bw Mutharika ni kaka wa rais wa zamani marehenu Bingu wa Mutharika.
 

Share this

Artikel Terkait

1 Response to "PETER MUTHARIKA ASHINDA UCHAGUZI WA MALAWI"

  1. Watch '90s MTV Video - Videodl.cc
    Video Tutorial: Watch '90s MTV Video. by YouTube. Play on your phone, tablet or desktop. free youtube to mp3 Search for: Movies, Sports, Movies.

    ReplyDelete