Mechi zilizochezwa
usiku wa kuamkia leo za Klabu Bingwa barani ulaya ambapo Manchester City
walianza vibaya michuano hiyo baada ya kupata kichapo cha goli moja bila majibu
kutoka kwa wenyeji wao Bayern Munich ya Ujerumani.
Goli la Bayern Munich
lilifungwa na Jerome Boateng katika dakika 90
Wakati Man City
wakiiadhibiwa ugenini na Bayern Munich, wenzao Chelsea wakiwa nyumbani Stamfode
Bridge walitoka na sare ya goli moja kwa moja na Schalke 04.
Bacelona wao waliamua
kuushikisha adabu Apoel ya Syprus kwa kuifunga goli moja bila majibu wakati FC
Porto ya Ureno wakifungulia mvua ya magoli iliyoambatana radi pale
ilipowanyeshea wapinzani wao Bate Borisov ya Belarus kwa jumla ya magoli 6 bila
majibu.
Matokeo mengine NK
Maribor ya Slovenia ilitoka sare ya 1 - 1 na Sporting Lisbon ya Ureno huku
Athletic Bilbao ya Hispania zikitoka uwanjani bila kufungana na Shaktar Donetsk
ya Ukraine.
AC Roma ya Italia wao
waliiadhibu CSKA Moscow ya Urusi kwa jumla ya magoli 5 -1 huku Ajax na Paris
St. Gamaine ya Ufaransa zikitoka sare ya moja kwa moja.
0 Comment to "MATOKEO YA UEFA CHAMPION LEAGUE"
Post a Comment