Wananchi wa Scotland wakiwa na mabango yao
Wananchi wakiwa kwenye foleni ya kupiga kula
Upigaji kura ya maoni nchini
Scotland unaendelea ambayo itaamua kama
nchi hiyo inaondoka kwenye muungano wake wa miaka 307 na Uingereza na kuwa
taifa huru.
Watu waliojitokeza
katika kura ya maoni wamekua wengi kwa sababu zaidi ya watu milioni 4 na laki
mbili walijiandikisha kupiga kura ambapo asilimia 97 ya watu hao wanastahili
kufanya hivyo.
Wananchi wanapiga kura
kwenye vituo 2,600 vya kupiga kura vilivyoko nchi nzima kwa kuchagua neno
“Ndio” au “Hapana” kwenye swali la kura ya maoni linalouliza kwamba “Ni vyema
Scotland iwe taifa huru?”.
Upande unaopinga
kujitenga kwa umoja huo unasihi kwamba kura ya “Ndio” itaharibu uchumi wa
Scotland na kuvuruga maisha ya kila mtu kama ushirika wa Uingereza ulioundwa
mwaka 1707 unavunjika.
0 Comment to "WANANCHI WA SCOTLAND WAPIGA KULA YA MAONI"
Post a Comment