Monday, November 5, 2012

UCHAGUZI WAANZA NCHINI MAREKANI


Rais Barack Obama ametoa wito wake wa mwisho kwa wapiga kura katika mkutano wa hadhara mjini Iowa huku wamarekani wakijitokeza kupiga kura kuamua ikiwa atapata muhula wa pili au mpinzani wake Mitt Romney ndiye atachukua usukani katika ikulu ya White House.
Kura za kwanza zimepigwa katika jimbo la New Hampshire, ambako inaarifiwa Obama na Romney wamepata kura tano kila mmoja kati ya kura kumi. Kura hizi hazitokani na wapiga kura kwa ujumla bali watu maalumu ambao huteuliwa kupiga kura katika kile kinachojulikana kama Electoral village.

Share this

Artikel Terkait

0 Comment to "UCHAGUZI WAANZA NCHINI MAREKANI"

Post a Comment