CHUO CHA KIU-DCC
KUSIMAMISHWA KUTOA MAFUNZO YA SHAHADA ZA UZAMILI NA UZAMIVU
Kampala International
University, Kampasi ya Dar-es-Salaam (KIU-DCC) kilichopo Gongo la Mboto,
Dar-Es-Salaam ni Chuo kilichopewa idhibati na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
(TCU). Kufuatia kuendesha mafunzo ya shahada ya Uzamili (Masters) na Shahada za
Uzamivu (PhD) kinyume cha utaratibu na kutokua na wahadhiri wa kutosha wenye
sifa stahili, Tume katika mkutano wake wa hivi karibuni ulikiamuru Kampala
International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam ifuatayo;
1. KIU isimamishe mara
moja mafunzo yote ya shahada za juu (Postgraduate) ikiwa ni pamoja na Shahada
za Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) katika kampasi ya
Dar-es-Salaam.
2. KIU ishirikiane na
wanafunzi wote iliyowadahili katika programu zilizotajwa hapo juu waweze
kuhamia kwenye vyuo vingine vyenye idhibati ya kutoa mafunzo hayo.
Tume haitatambua
shahada yeyote ya Uzamiili au Uzamivu itakayotolewa na chuo hicho kwa
watakaosoma katika kampasi ya Dar-es-Salaam. Angalizo:
Chuo cha KIU Kampasi ya
Dar-es-Salaam kina ithibati na kitaendelea kutoa mafunzo ya shahada ya kwanza
(Bachelors), Diploma au vyeti zilizopitishwa na TCU kwa mujibu wa Ithibati
husika tuu.
Imetolewa na:
Katibu Mtendaji
TUME YA VYUO VIKUU
TANZANIA (TCU)
0 Comment to "TCU WAKIFUNGIA CHUO CHA KAMPALA INTERNATIONAL UNIVERSITY ( KIU ) KWA KUTOKIDHI VIGEZO "
Post a Comment