Thursday, July 25, 2013

CHELSEA YAIFUNGA INDONESIA ALL STARS 8-1





Chelsea imemaliza ziara yake barani Asia kwa kuifungwa timu ya mastaa wa Indonesia  ”Indonesia  All-stars” mabao 8-1, lakini kikubwa zaidi kwake ni jinsi wachezaji wake vijana walivyoonesha kiwango cha juu na morali ya kufanya kazi naye.
Romelu Lukaku amedhihirisha utata wake wa kufumani nyavu baada ya kufunga mabao manne na mchezaji aliyeko katika majaribio Chelsea ameonesha uwezo baada ya kufunga bao leo katika dakika ya 50, hivyo kuendelea kujiwekea mazingira ya kusajliliwa na Mourinho.
Kevin De Bruyne alicheza kwa kiwango cha juu wakiwa Bangkok na  Kuala Lumpur, pia  Nathaniel Chalobah alionesha kiwango kikubwa  sana mjini Jakarta
Kikosi hicho cha Chelsea : Blackman (Schwarzer 46); Wallace (Ivanovic 46), Cahill, Terry (Kalas 46), Bertrand (Cole 46); Chalobah (Essien 46), Van Ginkel (McEachran 60); Ramires (Feruz 60), Hazard (Piazon 60), Moses (Traore 46); Ba (Lukaku 46).
Mabao yametiwa nyavuni na: Hazard (penalty) 21, Ramires 29, 56 Ba 32, Terry 45, Traore 50, Lukaku 52, 65.
Bao la Indonesia All-Stars limefungwa na Kalas (og)  katika dakika ya 67.

Share this

0 Comment to "CHELSEA YAIFUNGA INDONESIA ALL STARS 8-1"

Post a Comment