Mke
wa mjukuu wa mfalme wa Uingereza, Prince William amejifungua mtoto wa kiume
katika hospitali ya St.Mary's, Paddington Mashariki mwa mji wa London.
Katika
taarifa ya Kasri la kifalme la Kensington, Duchess wa Cambridge amepata mtoto
wake wa kwanza majira ya saa kumi na dakika ishirini na nne za jioni kwa saa
Uingereza,akiwa amezaliwa na kilo 3.62874.
Kasri
la Kifalme limesema, mama na mwanawe wanaendelea vyema na watasalia hospitalini
usiku huu.
Baba
wa Mtoto, Prince William alishuhudia wakati mtoto akizaliwa.
Tangazo
la kuzaliwa kwa mtoto limetolewa na kuonyeshwa mbele ya lango kuu la Kasri kuu
la kifalme la Uingereza la Buckingham kama utamaduni na mila za Uingereza
zilivyo.
Taarifa
rasmi iliyosainiwa na jopo la madaktari bingwa kuthibitisha kujifungua kwa
Duchess wa Cambridge ilipelekwa kwenye kasri la kifalme chini ya ulinzi wa
polisi.
Malkia
wa Uingereza,Duke wa Edinburgh, Prince wa Wales, Duchess wa Cornwall na Prince
Harry pamoja na wanandugu wa familia zote wametaarifiwa juu ya kujifungua
salama .
Waziri
Mkuu wa Uingereza, David Cameron ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter
ujumbe wa kuwapongeza Prince William na mkewe kwa kupata mtoto wa kiume na
kusema nchi nzima itashangilia kwa ujio wa mtoto wa kiume.
Kiongozi
wa chama cha Labour Ed Miliband pia ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa
Twitter "pongezi nyingi kwa Duke na Duchess wa Cambridge. Nawatakia wao na
mtoto wao furaha na afya njema."
0 Comment to "UFALME UINGEREZA WAPATA MTOTO WA KIUME"
Post a Comment