Klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa beki wa kimataifa
wa Ivory Cost Kolo Toure kutoka Manchester City.
Toure
mwenye miaka 32 amesajiliwa na Liverpool kwa mkataba wa miaka miwili baada ya
mkataba na Man City wanaomilikiwa na kampuni ya Etihad kumalizika.
Ameichezea
City jumla ya michezo 102 baada ya kusajiliwa akitokea Arsenal mwaka 2009 kwa
pound milioni 14, lakini alicheza mechi 18 pekee msimu uliopita na kujikuta
akiachwa kwenye kikosi cha wachezaji wa Man City walioshiriki michuano ya klabu
bingwa barani Ulaya.
Kolo
Toure anaenda Merseyside baada ya aliyekuwa nahodha msaidizi wa klabu hiyo
Jamie Carragher kutundika daruga huku hatma ya beki kitasa wa timu hiyo rais wa
Slovakia Martin Skrtel ikiwa haijulikani.
Ameuambia
mtandao wa klabu hiyo hatua hiyo ina maana kubwa kwake, na amejiunga na moja
klabu bora nchini England.
"Nilipoondoka
City ilikuwa ni muhimu kwangu kubaki England kwa kuwa ni ligi bora na kuja
Liverpool ni hatua kubwa kwangu."
"Nimeichagua
Liverpool kutokana na historia yake na hamasa ya wachezaji wanavyoitumikia timu
yao." Alisema Toure.
Katika
misimu saba aliyocheza Arsenal, Toure alishinda Kombe la FA mara mbili na
alikuwa miongoni mwa kikosi cha Arsenal ambacho kiliandika historia ya kucheza
ligi ya 2003-04 bila kufungwa hata mechi moja.
Toure
ni mchezaji wa nne kusajiliwa na Liverpool baada ya klabu hiyo kumsajili, Luis
Alberto na Lago Aspas pamoja na mlinda mlango Simon Mignolet aliyesajiliwa
akitokea Sunderland.
0 Comment to "LIVERPOOL WAMSAJILI KOLO TOURE"
Post a Comment