Nchi ya Cameroon wanatarajiwa kwenye
nchi Ulaya kuwashawishi wachezajiwa wa nchi hiyo wanachezea katika nchi za
ulaya kujiunga na timu ya taifa ya nchi hiyo "Indomitable Lions".
Mpango huo wa kusaka vipaji vipya
umekuja wakati Cameroon ikiwa inajiandaa kushiriki fainali za kombe la dunia
mwaka kesho nchini Brazil.
Chama cha soka cha Cameroon -
Fecafoot kimesema mpango wao kwa sasa ni kushawishi wachezaji wanne wanaocheza
soka ya kulipwa nchini Ufaransa.
Wachezaji hao Axel Ngando anachezea
klabu ya Auxerre ya ligi daraja la pili nchini Ufaransa, Samuel Umtiti
anachezea Lyon na Jean- Christophe Behebeck anachezea Valenciennes.
Mchezaji mwinginie anayewindwa ili
kuuongeza nguvu kwenye timu ya taifa ya Cameroon ni Paul Geoges Ntep de Madiba
ambaye pia naye anayechezea Auxerre ya Ufaransa.
Tunataka kuwashawishi hao wachezaji
wachezee timu ya taifa ya Cameroon, na hasa kwenye fainali za Kombe la Dunia na
pia wachezee Cameroon kwa hapo baadae Shirikisho la soka la Cameroon limesema
kwenye taarifa yake.
0 Comment to "CAMEROON KUKUSANYA WACHEJI WAKE WA ULAYA"
Post a Comment