Mchezaji wa Manchester City ambaye pia hucheza nafasi ya kiungo cha kati katika timu ya Ivory Coast, Yaya Toure ndiye mwanasoka bora zaidi mwaka 2013 barani Afrika
Toure alikabidhiwa tuzo
la (CAF) mwaka wa tatu mfululizo katika sherehe zilizofanyika mjini Lagos,
Nigeria Alhamisi usiku.
Aidha Toure pia
alishinda tuzo la BBC la mwanasoka bora zaidi barani Afrika mwaka jana.
Alikuwa anawania tuzo
hilo dhidi ya mchezaji mwenzake wa Ivory Coast Didier Drogba, ambaye huchezea
Galatasaray na John Mikel Obi mnigeria ambaye husakata soka nchini Uingereza.
"nimefurahi sana
kwa sababu hii ni ishara kuwa nacheza vyema sana ,'' alisema Toure baada ya
kupokea tuzo yake.
Lakini alisema kuwa
majaji walikuwa na wakati mgumu kumchagua mchezaji bora kwa sababu washindani
wenzake wote ni wazuri.
''Sikudhani kama
nitashinda kwa sababu Drogba na Obi Mikel ni wasakataji wazuri wa kabumbu,''
aliongeza Toure.
Abedi Pele wa Ghana
alishinda tuzo hiyo mara tatu kati ya mwaka 1991-93 huku Samuel Eto'o akishinda
kati ya mwaka 2003-05.
Bila shaka klabu ya Man
City anakosakatia kambumbu Toure, bado haishinda kombe lolote la klabu lakini
nyota yake imekuwa iking'aa sana nyumbani na katika nyanja za kimataifa.
Toure ndiye mchezaji
pekee wa kiafrika kuwa katika orodha ya wachezaji 23 walioteuliwa kuwania tuzo
la mchezaji bora la FIFA mwaka jana.
Mshindani wake wa
karibu aliyekuwa pia anawania tuzo la Caf, Mikel, mwenye umri wa miaka 26,
alisaidia Nigeria kushinda kombe la taifa bingwa Afrika mwaka 2013 nchini
Afrika Kusini.
0 Comment to "YAYA TOURE NDIYE MWANASOKA BORA ZAIDI MWAKA 2013 BARANI AFRIKA"
Post a Comment