Kajiuzuru kufuatia
shinikizo kali na kukosolewa kwa mwendo wake wa kujikokota katika kusuluhisha
mgogoro wa kidini unaotokota nchini humo.
Hatma ya Djotodia
ilikuwa swala kuu katika ajenda ya mkutano wa viongozi wa kikanda kuhusu mzozo
unaoendelea nchini humo.
Mkutano huo ulifanyika
nchini Chad huku maelfu wakiendelea kutoroka nchini humo kutokana na ghasia.
Maelfu ya watu
waliandamana leo katika barabara za mji mkuu Bangui kumtaka Rais Djotodia,
ajiuzulu.
Rais Djotodia
amekosolewa vikali kwa kukosa kumaliza mapigano ya kidini kati ya wakristo na
waliokuwa waasi waisilamu ambao walimsaidia kuingia mamlakani kwa njia ya
mapinduzi mwaka jana.
Baraza lote la mpito
katika Jamuhuri ya Afrika ya kati limekwenda nchini Chad ambako viongozi wa
Afrika wanakutana kujadili mzozo unaoendelea nchini humo.
Mkutano huo wa viongozi
wa kikanda, uliahirishwa, mapema asubuhi Ijumaa.
Lakini wajumbe kwenye
mkutano huo wanasema walitakiwa kuendelea na mkutano usiku kucha ili kubuni
mkakati kuhusu mustakabali wa Djotodia.
Viongozi wa kikanda
wanasema wajumbe mia moja na thelathini na watano waliitwa kwa mkutano huo kwa
sababu ni raia wa nchi hiyo pekee wanaoweza kuamua hatma ya taifa lao.
Ghasia baina ya
wanamgambo wa kiisilamu na kikristo zimesababisha maelfu ya watu kuyahama
makazi yao.
Djotodia aliingia
mamlakani baada ya mapinduzi ya kijeshi mwezi Machi mwaka jana hali iliyotumbukiza
taifa hilo katika viya vya wenyewe kwa kwenyewe.
tunamsubiria na Pinda asepe
ReplyDelete