Saturday, August 24, 2013

ZITTO KABWE: BALOZI ZA TANZANIA ZINATUMIA FEDHA VIBAYA




Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali na mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe amesema balozi karibu zote za Tanzania zina utumiaji mbaya wa fedha za umma yaani matumizi bila utaratibu  kufuatwa.

Ameeleza kwamba tatizo lililopo ni tatizo la kimfumo au kimuundo hususan kwenye wizara ya mambo ya nje na kujikuta mahesabu ya balozi yamekuwa na matatizo.

Kwahiyo anaeleza kuwa kamati yake ilichofanya kwanza imeagiza ukaguzi maalum kwa wizara ya mambo ya nje  ili pia mdhibiti mkuu na mkaguzi wa hesabu za serikali awasilishe kitu kinachoitwa ukaguzi wa mfumo ili kuweza kujua ni nini kamati yake inaweza kufanya  ili wizara ya mambo ya nje isiwe na hoja za ukaguzi nyingi kama ambavyo imetokea hivi sasa.




Alizitaja balozi za Washington Dc, New York, Canada , Berlin, Malaysia,Brussels, London, New Delhi na Beijing kuwa na matatizo zaidi
 

Share this

Artikel Terkait

0 Comment to "ZITTO KABWE: BALOZI ZA TANZANIA ZINATUMIA FEDHA VIBAYA"

Post a Comment