Ofisi zaidi ya 12 za mabalozi wa Marekani katika Mashariki
ya Kati na Afrika Kaskazini zimefungwa.
Hatua
hiyo inafuatia serikali ya Marekani kusema Ijumaa kwamba inaamini kuwa al-Qaeda
au kundi linaloshirikiana na al-Qaeda huenda likawa linapanga mashambulio.
Ubalozi
wa Marekani mjini Kabul piya umefungwa kwa sababu ya ilani hiyo kuhusu usalama.
Mataifa
kadha ya Ulaya nayo yamefuata - Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimesema kuwa
balozi zao mjini Sanaa, Yemen, zitafungwa mwisho wa juma.
0 Comment to "BALOZI ZA MAREKANI KUFUNGWA"
Post a Comment