Saturday, August 24, 2013

MSIMU WA LIGI KUU TANZANIA YANGA YAANZA VYEMA




Msimu wa 2013/2014 wa ligi kuu soka Tanzania bara umeanza wakati timu 14 zilishuka dimbani jana.

Mechi zilizokuwa zikiangaliwa sana ni zile za timu zilizoshika nafasi tatu za juu msimu uliopita yaani mabingwa Yanga, washindi wa pili, Azam Fc na mshindi wa tatu, Simba Sc.

Tayari kumekucha kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, klabu ya Yanga ambao wameanza kwa uzuri kampeni za kutetea ndoo yao, baada ya kuwatwanga wageni wa ligi hiyo, Ashanti United ‘Watoto wa Jiji’ kwa mabao 5-1 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga leo yalifungwa na Jerry Tegete dakika za 10 na 57, Simon Msuva dakika ya 47, Haruna Niyonzima dakika ya 73 na Nizar Khalfan dakika ya 90, wakati bao pekee la Ashanti lilifungwa na Shaaban Juma dakika ya 89.

Pia mchezo kati ya samba na Rhino Ranger ilikua droo ya 2 -2 na Mtibwa Suger na azam sare 1-1

Share this

Artikel Terkait

0 Comment to "MSIMU WA LIGI KUU TANZANIA YANGA YAANZA VYEMA"

Post a Comment