Mlemavu mmoja kutoka Denmark Dennis Aabo amekuwa binadamu wa kwanza kupewa mkono wa kieletroniki wenye hisia kama ule wa binadamu.
Mkono wa kielektroniki
Katika
tukio linalopigiwa upatu kuimarisha hali ya walemavu katika siku za usoni,
madaktari huko Italia wameuunganisha mkono huo wa kielektroniki na neva za
mabaki ya mkono wa Dennis uliokatwa baada ya ajali mbaya ya fataki na hivyo
kumwezesha kuhisi kupitia kwa vidole vya mkono huo wa kielektroniki.
Silvestro
Micera aliyeongoza upasuaji huo alifurahishwa mno na uwezo wa mgonjwa wake
kuutumia mkono huo bandia .
''
tumeshangazwa sana na urahisi wa mgonjwa wetu kuwasiliana mara moja na mkono
huu bandia wa kielektroniki kuekelea majukumu ya kushika na kuhisi vitu tofauti
.
Hata
ikiwa upasuaji huu utakuwa wa muda tu, ninahakika Denis ameotambua mwenyewe
kuwa utakuwa wenye manufaa makubwa kwake katika siku za usoni''
Dennis
hakuficha furaha yake alisema mkono huo umebadilisha kabisa hali yake.
''hisia
zangu za mkono zimeimarika maradufu maanake ninawezajua ugumu na mfumo wa kitu
chochote ni kama mkono wa kawaida''
0 Comment to "MLEMAVU WA KWANZA KUTUMIA MKONO WA KIELECTRONIKI"
Post a Comment