Wednesday, December 5, 2012

UHURU MARATHON YAZINDULIWA RASMI

Mbio mpya za Nyika za Uhuru 'Uhuru Marathon' zimezinduliwa jana jijini Dar es Salaam naWaziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara. Pichani ni Waziri akiangalia nembo ya Mashindano hayo mapya yatakayo kuwa yakifanyika Desemba 8, ya kila mwaka kuuenzi uhuru wa Tanzania. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa Intelecture Communication Ltd, Waandaaji wa Mbio hizo, Innocent Meleck.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akizindua rasmi tovuti ya Mbio hizo ya http://www.uhurumarathon.com pamoja nae ni Mkurugenzi wa Intelecture Communication Ltd, Waandaaji wa Mbio hizo, Innocent Meleck.


Dk. Fenela Mukangara akizungumza.

 Mkurugenzi wa Intelecture Communication Ltd, Waandaaji wa Mbio hizo, Innocent Meleck akitoa maelezo juu ya Mashindano hayo.


Mrisho Mpoto 'Mjomba' akighani mashairi yake kama kawaida.

Waimbaji wa Bendi ya Mjomba, kutoka  kushoto ni Josephina Johnswam, Ismail Kipira na Twaha Farahani wakiwajibika wakati wa Uzinduzi huo.
Habari na: Father Kidevu

Share this

Artikel Terkait

0 Comment to "UHURU MARATHON YAZINDULIWA RASMI"

Post a Comment