Familia
ya mwanariadha mlemavu nchini Afrika Kusini, Oscar Pistorius, wameshstushwa na
picha zilizofichuliwa za bafu alimomuulia mpenzi wake mnamo mwezi Februari.
Shirika
la habari la Uingereza la Sky, mnamo Ijumaa, lilionyesha picha za kuogofya
zinazoshukiwa kuwa za bafu ambalo mpenzi wa Pistorius Reeva Steenkamp, aliuawa.
Polisi walisema kuwa wamechukizwa mno na kufichuliwa kwa picha hizo.
Bwana
Pistorius mwenyewe anakanusha madai ya kumuua mpenzi wake, kupitia mlango wa
bafu alimokuwa , alisema alidhani kuwa alikuwa mwizi aliyevamia nyumba yake.
Anatarajiwa
kufikishwa mahakamani kwa hatua ya mahakama mwanzo kutathmini kesi siku yake
Jumanne.
Pistorius
ni mwanariadha mlevamu asiye na miguu yake miwili ingawa hukimbia kwa miguu
bandia au vyuma. Alishiriki michezo ya Olimpiki mjini London mwaka jana.
''Familia
ya Pistorius ilimuunga mkono alipokuwa anajiandaa kufikishwa mahakamani ,
alisema mjomba wake,'' Arnold Pistorius.
''Tunaamini
maneno yake , tunampenda na tutamuunga mkono kwa kila hatua ya kesi
hii,''alisema Mjombake Pistorius. "tumeshtushwa na picha hizi za ajali
iliyotokea nyumbani kwa Oscar."
Msemaji
wa polisi ameelezea kuwa polisi wanachunguza nani aliyefichua picha hizo . ''Kitendo
hiki hakikuhitajika na kimetuudhi kweli. Hatujui picha hizi zimetoka wapi,''
alisema polisi huyo.
Pistorius
atafikishwa mahakamani Jumanne kwa mara ya kwanza tangu kuachiliwa kwa dhamana,
kufuatia kukamatwa kwake, kuhusu mauaji ya Steenkamp.
Kesi
hiyo inatarajiwa kuakhirishwa kwani uchunguzi wa polisi ungali unaendelea.
Pistorius
ameajiri baadhi ya mawaklili shupavu nchini Afrika Kusini kumtetea. Anasema
kuwa alimpiga risasi Bi Steenkamp kupitia mlango wa choo kimakosa baada ya
kudhani alikuwa mwizi.
Hata
hivyo, viongozi wa mashtaka wanasema kuwa alimuua kwa maksudi baada ya wawili
hao kugombana.
0 Comment to "FAMILIA YA PISTORIUS YASHTUSHWA NA PICHA"
Post a Comment