Mshambulizi matata wa
Barcelona Lionel Messi na babake wanachunguzwa nchini Uhispania kwa kuilaghai
serikali ya nchi hiyo zaidi ya pauni milioni tatu nukta nne.
Mchezaji huyo kutoka
Argentina na babake, Jorge wanatuhumiwa kuibia serikali ya nchi hiyo, kwa
kujaza fomu zizizokuwa za ukweli za marejesho ya kodi kati ya mwaka wa 2007 na
2009.
Hata hivyo mechezaji
huyo mwenye umri wa miaka ishirini na mitano hajasema lolote kuhusiana na madai
hayo.
Messi hulipwa Euro
milioni kumi na sita kila mwaka na ndiye mchezaji anayelipwa kiasi cha juu
zaidi duniani.
Lakini mwendesha
mashtaka Raquel Amado, aliwasilisha nyaraka za mahakama nyumbani kwake kwa
mchezaji huyo katika mtaa wa kifahari wa Gava mjini Barcelona.
Jaji mjini humo ni
sharti waidhinisha malalamishi dhidi ya mshukiwa yeyote kabla hajafunguliwa
mashtaka.
Messi na babake
wanashukiwa kutumia kampuni katika mataifa ya ngambo, mjini Belize na Uruguay
kuuza haki za kutumia picha ya mchezaji huyo.
Mchezaji huyo na babake
wanatuhumiwa kutumia kampuni hizo zilizoko nje ya Uhispania, ambako anaishi na
kucheza soka ya kulipwa, kukwepa kulipa kodi inayokisiwa kuwa pauni milioni
tatu na nusu.
0 Comment to "LIONEL MESSI NA BABA YAKE WANACHUNGUZWA NCHINI UHISPANIA KWA KUILAGHAI SERIKALI"
Post a Comment