Harambee
Stars imeondolewa kwenye kinyang'anyiro cha kufuzu kombe la dunia 2014
Mchuano
wa kufa na kupona ulishuhudiwa kati ya bingwa wa Afrika Super Eagles wa Nigeria
na Harambee Stars wa Kenya katika uwanja wa kimataifa wa Moi Kasarani mjini
Nairobi.
Musa
Ahmed aifungia Nigeria bao la kwanza na la pekee kunako dakika ya 81. Mashabiki
wa Kenya Kimya!
Baadhi
ya mashabiki wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars waanza kuondoka uwanjani.
Mashabiki
wa Nigeria hawakuwa wengi uwanjani wakikisiwa kufika 300, lakini licha ya
uchache wao ,hawakufa moyo.Mandishi wa BBC Odeo Sirari aliyekuwa
uwanjani,alishuhudia mashabiki wachache wa Nigeria wakiisiahngilia timu yao kwa
nyimbo na ngoma japo hawakuwa wanasikika kutokana na mayowe ya wakenya.
Ilikuwa
mechi ya mkondo wa pili kwa timu hizo mbili baada ya kwenda sare ya bao moja
kwa moja walipocheza kwa mkondo wa kwanza mjini Calabar Nigeria mwezi jana.
Mechi
hii ni ya kundi la F ya kugombania nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la
Dunia mwakani nchini Brazil.
Vijana
wa kocha Stephen Keshi, wanatarajiwa kuendeleza ushindi wao hii leo
wakijitafutia nafasi ya kuwakilisha Afrika katika michauno ya kombe la dunia
nchini Brazil
Kwa
vijana wa Eagles wanaosemekana kujiandaa vyema, wanafahamu kuwa ikiwa
watashindwa basi itakuwa hasara kwao kwani hawataweza kwenda Brazil.
Licha
ya kwenda sare mwezi jana, Nigeria inaingia kwenye mkondo huu bila ya kushindwa
mechi yoyote ya makundi kati ya kumi na sita zilizocheza hadi kufikia sasa.
Wadadisi
wanasema Eagles wanaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kushinda. Mwandishi
wetu Odeo Sirari alipiga kambi katika uwanja wa Moi Kasarani kutupasha mambo
yalivyokuwa.
14:50
PM :Shamra shamra zimeanza kupamba moto katika uwanja wa kimataifa wa Moi
Kasarani. Mwandishi wa BBC ambaye yuko katika uwanja huo Odeo Sirari, anasema
kuw mashabiki wanzidi kumiminika uwanjani. Milango ya uwanja ilifunguliwa rasmi
majira ya saa tano asubuhi
14:58
PM: Mojawapo ya mabango ya mashabiki uwanjani yana bendera ya Kenya na
maandishi ''Oga you are finished'' kwa maana kuwa Nigeria itashindwa . Odeo
anasema hayo ni maoni ya mashabiki wa Nigeria uwanjani
Timu
zote zina mbili zina uhakika zitashinda mechi ya leo. Tuache tuone msema kweli
Mechi
inatarajiwa kuanza saa kumi kamili. Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuhudhuria
15:43
PM: Mashabiki washangilia wachezaji wa Harambe Starrs wakiingia uwanjani. Super
Eagles nao pia wameingia uwanjani . Wachezaji wa pande zote mbili sasa
wanapasha misuli joto
15:48
PM: Uwanja wa michezo wa Moi Kasarani una uwezo wa kushenei mashabiki takriban
60,000
15:49
PM: Kikosi cha Harambe Stars: Mlinda lango Duncan Ocheng, Safu ya ulinzi David
Owino Brian Mandela David Ochieng . Wachezaji wa kiungo cha kati Mulinge Ndeto,
Victor Wanyama Jamal Mohammed,Johana Omolo na Peter Opiyo. Washambulizi ni Kefa
Aswani na Fracis Kahata
16:07
PM: Mechi imeng'oa nanga rasmi . Kikosi cha Eagles...Efe, Oboabona, Omeroo
Elderson, Onazi, Mikel, Mba,Oduamadi,Musa, Ideye Golikipa ni Enyeama
16:33
PM baada ya mechi kuchezwa kwa zaidi ya dakika thelathini bado timu hizo ziko
sare tasa
16:41
Mshambuliaji wa Kenya Kepha Aswani anenekana akichechema uwanjani na kuwa
mashabiki wanataka aondolewe
16:51
Shambulizi katika eneo la hatari lango la timu ya Kenya. Sunday Mba aliupiga
mpira kwa kichwa lakini ukapaa juu ya mlingoti wa goli . Mashabiki wa Kenya
wabaki kimya
17:27
pm Peter Opiyp atekeleza shambulizi lango la Nigeria.
17:28
Nigeria yafanya mabadiliko, SundayMba aondolewa
17:28
Victor Wanyama apata jeraha..anahudumiwa. Kenya yashambulia, Kombora la Johhana
Ngeno lapaa juu ya mlingoti kunako dakika ya 56. Victor Wanyama arejea
uwanjani, mashabiki wa kenya washangilia. Nigeria inahitaji ushindi katika
mechi hii dhidi ya Kenya ili kusonga mbele. Sare ya kutofungana itaipa Kenya
nafasi nzuri ya kusonga mbele
17:38
pm: Mlinzi wa kati wa Harambee Stars Brian Mandela afanya kazi ya ziada
kupangua makombora ya wa Nigeria.
Mashabiki
wa Kenya wanaimba: '' Haki yetu! Bao! Haki yetu! bao!
Victor
wanyama aondoka tena uwanjani, yamkini jeraha lake ni baya.
Timu
ya taifa ya Nigeria yafanya mabadiliko dakika ya 64 anaondoka Brown Aye
anaingia Ujah Antony
17:39
pm: Victor Wanyama arejea tena uwanjani licha ya kuonekana amejeruhiwa.
Mashabiki wa Kenya wanataka aendelee kucheza.
17:40
Mulinge Munandi aonyeshwe kadi ya njano kwa kumfanyia masihara mchezaji wa
Nigeria Musa Ahmed. Harambee stars yazidisha shinikizo dhidi ya Super Eagles.
Mashabiki wakosa subira.. wanaimba haki yetu! bao! haki yetu! bao.....
Peter
Opiyo wa harambee stars aondolewa, Patrick Osiako aingia uwanjani.
17:52
pm: Mashabiki wa timu ya taifa ya Nigeria kama mia 200 hivi washangilia bao
lililofungwa na Musa Ahmed. Baadhi ya mashabiki wa Kenya wawazomea wenzao wa
Nigeria kwa kuwarushia chupa za maji.
Safu
ya mashambulizi ya Harambee stars yaonekana kufifia.
Dakika
ya 87, Oduamani wa Nigeria aondoka anaingia Ogude.
Nigeria
yapata kona ya pili kipindi cha lala salama
0 Comment to " HARAMBEE STARS IMEONDOLEWA KINYANG'ANYIRO CHA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2014"
Post a Comment