Real Madrid ya Hispania na Manchester United ya England
zimetoka sare baada ya kufungana bao moja kwa moja katika mchezo wa mabingwa
barani Ulaya, UEFA, uliochezwa katika uwanja wa Real Madrid, Bernabeau.
Manchester United United ndiyo iliyokuwa ya kwanza kufunga goli katika dakika
ya 20 ya mchezo, baada ya Danny Welbeck kufunga kwa kichwa mpira wa Kona. Hata
hivyo furaha ya Manchester United ilidumu kwa dakika kumi tu, kwani katika
dakika ya 30 Christian Ronaldo iliisawazishia timu yake goli alilofunga kwa
kichwa baada ya mpira wa adhabu ndogo.
Baada ya hapo timu zote ziliendelea kushambuliana hadi mapumziko, huku Real
Madrid ndiyo ikitawala zaidi mpira na Manchester United ikifanya mashambulio ya
kushtukiza.
Kipindi cha pili kilianza kwa Manchester United kushambulia lango la Real
Madrid, hata hivyo mashambulio yaliigeukia Manchester United, huku mlinda mlango
wake David de Gea akiokoa michomo mingi kutoka kwa vijana wa Real Madrid.
Manchester United ilikuwa na bahati kupona kipigo kutoka kwa vijana wa
Mourinho, kutokana na kuumiliki mpira muda mrefu na kupeleka mashambulio ya mara
kwa mara kiasi kwamba D e Gea alifanya kazi kubwa ya kuokoa michomo hiyo.
Alipoulizwa Mourinho kuhusu mpambano huo, anasema vijana wake walitawala
mchezo huo, huku wapinzani wao wakisubiri kufanya mashambuliuo ya kushtukiza. Na
kwa upande wa kumiliki mpira, Mourinho alisema timu zote zilicheza asilimia 50
kwa 50.
Hata hivyo kwa mujibu wa takwimu za mchezo huo, Real Madrid ilitawala kwa
asilimia 54 dhidi ya 46.
Katika mchezo mwingine wa michuano hiyo, Shakhtar Donetsk ya Ukraine imetoka
sare ya 2-2 na Borussia Dortmund ya Ujerumani.
0 Comment to "REAL MADRID, MANCHESTER UNITED SARE"
Post a Comment