England wametoka
Sare ya 0-0 na Ukraine huko Kiev na kujikita kileleni mwa Kundi
HENGLAND-LAMPARD_N_GERRARD la kuwania kufuzu kwenda Brazil Mwaka 2014 kwenye
Fainali za Kombe la Dunia.
Zikiwa zimebaki
Mechi mbili kwa kila Timu kwenye Kundi H, ambapo Mshindi wa Kundi pekee ndie
anakwenda Brazil na Mshindi wa Pili anaangukia Mechi ya Mchujo, England
wanaongoza Kundi kwa Pointi moja mbele ya Ukraine na Montenegro huku wakiwa na
Mechi mbili za Nyumbani Uwanja wa Wembley zitakazochezwa Oktoba.
Mechi hizo za
England ni dhidi ya Montenegro na Poland.
Katika Mechi
nyingine ya Kundi H iliyochezwa leo, Poland wamewatwanga San Marino Bao 5-1.
NETHERLANDS na
ITALY pia zimefanikiwa jana kuwa nchi za kwanza kutoka Barani Ulaya kufuzu
kwenda kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwakani.
Timu ambazo
tayari zipo fainali za kombe la dunia:
· BRAZIL==WENYEJI
· JAPAN
· AUSTRALIA
· IRAN
· SOUTH KOREA
· ITALY
· NETHERLANDS
0 Comment to "UKRAINE VS. ENGLAND: DROO 0-0"
Post a Comment