Rais wa Sudan Omar al Bashir anatishia kufunga bomba
linalobeba mafuta kutoka Sudan Kusini kwenda kaskazini , anasema kusini inaunga
mkono waasi.
Bw.Bashir alisema katika hotuba ya Televisheni
Jumatatu kwamba Sudan itafunga bomba hilo
la mafuta, kama Sudan Kusini itawapa uungaji mkono wa aina yeyote waasi,
katika maeneo ya mpakani ya Kordofan
Kusini na Blue Nile na eneo lenye utete
mkubwa la magharibi la Darfur.
Rais huyo akilindwa
na maafisa wa jeshi, alizungumza
baada ya jeshi kusema limechukua tena mji wa Abou Kershola kutoka kwa
waasi huko Kordofan Kusini.
0 Comment to "RAIS OMAR AL BASHIR ANATISHIA KUFUNGA BOMBA LA MAFUTA"
Post a Comment