Klabu ya Barcelona, imekubali kumsajili
mshambuliaji matata kutoka Brazil Neymar kutoka kwa klabu ya Santos.
Mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 21, anatarajia kukamilisha uasajili huo siku ya Jumatatu.
Kwa mujibu wa
taarifa kutoka Barcelona, vilabu hivyo viwili vimeafikiana kuhusu usajili wa
mchezaji huyo.
Barcelona imemtaja
mshambuliaji huyo kama mchezaji ambaye ana uwezo wa kuwa bora zaidi duniani.
Katika mtandao
wake wa kijamii wa Instagram, Neymar, alichapisha ripoti kuthibitisha usajili
huo na kuwashukuru mashabiki wa Santos, kwa kumuunga mkono katika kipindi cha
miaka tisa iliyopita.
Katika taarifa
hiyo iliyoandikwa kwa lugha ya Kireno, Neymar, alisema licha ya kuondoka daima
moyo wake utasilia na klabu hiyo.
Awali kulikuwa na
fununu kuwa klabu ya Real Madrid, vile vile ilikuwa na nia ya kumsajili
mchezaji huyo ambaye mkataba wake na Santos ungemalizika msimu ujao.
Neymar atachecheza
mechi yake ya mwisho siku ya Jumapili dhidi ya Flamengo, kabla ya kujiunga na
Bercelona baada ya fainali za kombe la Shirikisho, ambayo itachezwa kuanzia
tarehe kumi na tano hadi thelathini mwezi ujao nchini Brazil.
Katika habari
zingine, mshambuliaji matata wa Manchester City Sergio Aquero, amesaini mkataba
mpya ambao utaongeza muda wake kwa mwaka mmoja zaidi.
0 Comment to "BARCELONA YAMSAJILI NEYMAR"
Post a Comment