Matokeo ya mapema ya
uchaguzi wa urais nchini Kenya yanaonyesha Uhuru Kenyatta ameshinda na kuepuka
raundi ya pili ya uchaguzi. Takwimu kutoka tume ya uchaguzi zinasema Kenyatta
ameshinda asilimia hamsini nukta tatu za kura zote zilizopigwa.
Lakini tume ya uchaguzi
itakagua hesabu hiyo kabla ya kutangaza matokeo baadaye leo jumamosi, siku tano
baada yawakenya kupiga kura. Uhuru amepata asilimia hamsini nukta sufuri tatu
na kuzuia kutokea kwa duru ya pili ya uchaguzi.
Matokeo yaliyotolewa na
tume ya uchaguzi yanaonyesha kuwa Uhuru alipata kura 6,173,433 huku mpinzani
wake Raila Odinga akipata 5,340,546
Kenyatta anakabiliwa na
mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC kuhusiana na ghasia za baada ya
uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007.
Waandishi wa BBC
wanasema iwapo Kenyatta atakabidhiwa ushindi katika raundi ya kwanza, mpinzani
wake waziri Mkuu Raila Odinga atakwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.
Tume ya uchaguzi
itatangaza matokeo rasmi ya mshindi baadaye leo. Tume hiyo pia itatangaza
mshindi wa uchaguzi huo na vile vile kama mshindi huyo ametimiza masharti ya
kikatiba ya kutangazwa kuwa rais wa nne wa Kenya.
Kamishna Yusuf Nzibo
alitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume Isaack Hassan.
Vile vile mgombea huyo
pia lazima awe ameshinda asilimia 25% katika nusu ya County zote 47 nchini
kenya.
Awali Waziri Mkuu Raila
Odinga alikuwa amewaalika waandishi wa habari nyumbani kwake kwa mkutano maalum
ili azungumzie maswala ya matokeo ya urais lakini baadaye mkutano huo
uliakhirishwa hadi siku ya Jumamosi , baada ya tume ya uchaguzi kutoa tangazo
lake la mwisho.
Habari na:BBC Swahili
0 Comment to "HESABU ZA KURA ZAMPA USHINDI KENYATTA"
Post a Comment