Ubao wa Matokeo
unavyosomeka mara baada ya kumalizika kwa mechi kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania
(Taifa Stars) dhidi ya Timu ya Taifa ya
Morocco
Kikosi cha kwanza cha Taifa Stars kilichocheza dhidi ya Morocco. Mpaka mwisho Taifa Stars 3 Morocco 1
Timu
ya Taifa ya Soka ya Tanzania kwa upande wa wanaume, Taifa Stars, jana imewapa
watanzania raha ya aina yake baada ya kuichabanga timu ya Morocco (Atlas Lions)
kwa jumla ya magoli 3-1 katika mchezo wa kuwania tiketi ya kwenda kwenye
fainali za Kombe La Dunia zitakazofanyikia nchini Brazil hapo mwakani. Ushindi
huo wa kishindo umepatikana katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa
jijini Dar-es-salaam.
Magoli
ya Taifa Stars yaliwekwa kimiani na wachezaji Thomas Ulimwengu kunako dakika ya
46 ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Mwinyi Kazimoto. Magoli mengine yaliwekwa
wavuni kupitia kwa Mbwana Samatta kunako dakika za 67 na 80 za mchezo. Thomas
Ulimwengu na Mbwana Samatta wote ni wachezaji wa kulipwa wanaochezea timu ya TP
Mazembe huko Congo DRC. Goli la kufutia machozi la Morocco lilifungwa na Youssef
El-Arabi kunako dakika ya 94.
Kwa
matokeo hayo, Taifa Stars hivi sasa inashika nafasi ya pili katika kundi (Kundi
C) kwa kuwa na pointi 6 ikiwa ni pointi moja pungufu kutoka kwa Ivory Coast
wanaoongoza kundi hilo. Morocco ni ya tatu ikiwa na pointi 2 wakati Gambia
inashika mkia ikiwa na pointi 1
0 Comment to "TAIFA STARS YAIADHIBU MOROCO 3 - 1"
Post a Comment