Moshi
mweusi umetokea kwenye dari la hekalu ya Sistine mjini Roma, kumaanisha kuwa
makadinali walioko ndani ya hekalu wameshindwa kuafikiana juu ya Papa mpya
anayetarajiwa kuchaguliwa.
Moshi
mweupe utaashiria kupatikana kiongozi mpya wa kanisa Katoliki la Roma.
Makadinali
hao wanatarajiwa kupiga kura mara nne kwa siku hadi pale thuluthi mbili ya
makadinali wote watakapoafikiana juu ya Papa mpya.
Walipiga
kura yao ya kwanza ambayo haikuleta maafikiano hapo usiku wa Jumanne. Yeyote
atakayeteuliwa kuliongoza kanisa hilo katoliki anakabiliwa na wakati mgumu,
ambapo kanisa limezongwa na kashfa mbali mbali pamoja na migawanyiko ya ndani.
Papa
aliyeondoka Benedikt wa Kumi na sita aliwashangaza wengi alipotangaza kujiuzulu
wadhifa huo miaka minane tu tangu kuchaguliwa. Yeye ndiye Papa wa kwanza
kujiuzulu katika miaka 600 ya historia ya kanisa hilo.
Alitoa
sababu kuwa amezeeka na afya yake imedhoofika kwa hivyo haoni kuwa anaweza
kutekeleza wajibu wake kikamilifu kama Papa wa kanisa.
0 Comment to "MOSHI MWEUSI VATICAN UKIASHILIA PAPA HAJAPATIKANA"
Post a Comment