Sunday, March 24, 2013

RAIS JINPING AKUTANA NA KIKWETE DAR-ES-SALAAM

 
Rais Xi Jinping, rais wa Uchina, ametia saini mikataba kadha na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania mjini Dar-es-salaam.
Rais Xi aliingia Dar-es-salaam akitokea Moscow ambako ndiko alikoanza safari yake ya kwanza katika nchi za nje tangu kutawazwa rasmi kuwa rais hivi karibuni.
 
Hapo awali alipokelewa kwa ngoma na mizinga.
 
Rais Xi alitia saini mikataba 17 ya uchumi na utamaduni, mojawapo ni kuhusu ujenzi wa bandari mpya Bagamoyo pamoja na reli itayoungana na reli nyengine za Tanzania.
 
Akizungumza ikulu mjini Dar-es-salaam, kiongozi wa Uchina alisema ziara yake ni ishara ya uhusiano mwema kati ya nchi mbili hizo ambao umeendelea tangu ulipoanza wakati wa Rais Julius Nyerere na Mao Zedong.
 
Safari yake barani Afrika inaonesha umuhimu wa Afrika kwa Uchina, kuwa ni chanzo cha madini na nishati na piya soko kwa bidhaa za Uchina.
 
Rais wa Uchina anatarajiwa kutoa hotuba muhimu leo Jumatatu kuhusu uhusiano baina ya Uchina na Afrika.
 
Uchina ni ya pili katika uwekezaji nchini Tanzania, baada ya Uingereza.
 
Bwana Xi piya anapanga kuzuru Afrika Kusini ambako viongozi wa mataifa ya uchumi unaochipukia, BRICS, watakutana Jumaane mjini Durban.
 
Baada ya hapo anapanga kuzuru Congo.

Share this

0 Comment to "RAIS JINPING AKUTANA NA KIKWETE DAR-ES-SALAAM"

Post a Comment