Thursday, March 21, 2013

MASHUA YAZAMA KATIKA PWANI YA NIGERIA


Mashua iliyokuwa imebeba watu 160 imezama umbali wa kilometa 74 toka pwani ya Nigeria, wanaosimamia shughuli za uokoaji wamesema.

Mashua hiyo, iliyoundwa kwa mbao, ilianzia safari yake huko kusini-mashariki mwa Nigeria Ijumaa, ikielekea Gabon, safari kati ya Afrika Magharibi na Kati inayopendwa na wafanyibiasahara wengi.


Tomi Oladipo wa BCC, akiwa mjini Lagos, anasema kwamba safari hizi huchukua siku kadhaa, na huwa si salama sana. Kwa ajili hiyo ajali hutokea mara kwa mara.


Mashua hiyo ilianzia safari mjini Oron, jimboni Cross River, na ilikuwa inasafiri katika Ghuba la Guinea ilipozama, duru rasmi zimesema.
 

Waokoaji waliokuwa karibu na mji mkuu wa Jimbo la Cross River, Calabar, walisema wameokoa makumi ya maiti ya wasafiri waliokufa maji.


Wawili wa walionusurika, mvulana mdogo na mwanamke, walishikilia silinda ya gesi kabla ya kuokolewa na wavuvi, afisadharura wa Jimbo la Cross River, David Akate, aliliambia shirika la habari la Reuters.

Share this

0 Comment to "MASHUA YAZAMA KATIKA PWANI YA NIGERIA"

Post a Comment