Shughuli ya kuhesabu kura za uchaguzi wa urais
nchini Kenya, ilisimamishwa usiku kucha kwa sababu ya hitilafu za mitambo ya
tume huru ya uchaguzi na mipaka iliyokuwa inatumika kwa mara ya kwanza katika
uchaguzi wa Kenya.
Maafisa wa tume hiyo, wamelazimika kusafiri kwa
barabara kutoka umbali wa maelfu ya kilomita ili kwenda katika kituo cha
kutangazia matokeo ya kura za urais mjini Nairobi kuwasilisha fumo zao za
matokeo.
Mfumo wa Elektroniki, tayari umekosolewa vikali kwa
kusababisha kuharibika kwa kura nyingi, zikikisiwa kuwa zaidi la laki tatu.
Maafisa wa uchaguzi wametoa wito wa utulivu na amani
kwa wakenya wakati tume ikiendelea kutatua tatizo la kura.
Naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta,ambaye anatakikana
na mahakama ya ICC kwa uhalifu dhidi ya binadamu, wakati wa ghasia za baada ya
uchaguzi Kenya, miaka mitano iliyopita, angalia yuko mbele katika matokeo ya
uchaguzi wa urais.
Kufikia sasa asilimia 42 ya kura za urais nchini
Kenya zimehesabiwa na kuwasilishwa rasmi kwa tume ya uchaguzi IEBC kupitia
mitambo ya electroniki.
Hata hivyo kumekuwepo malalamishi kuhusu
kucheleweshwa kwa shughuli ya kujumlisha kura kutokana na hitilafu ya mitambo.
Uhuru Kenyatta, anayekabiliwa na kesi katika mahakama
ya uhalifu wa kivita ICC, angali anashikilia uongozi huku kura za urais zikiwa
bado zinahesabiwa.
Huu ni uchaguzi mkuu wa kwanza kufanyika tangu
ghasia za baada ya mwaka 2007/2008 kufuatia matokeo yaliyozua utata.
Kenyatta aliendelea kuwa mbele kwa hesabu ya matokeo
ya mwanzo dhidi ya mpinzani wake waziri mkuu Raila Odinga katika siku ya pili
ya shughuli ya kuhesabu kura zaidi ya masaa 36 baada ya shughili ya upigaji
kura kukamilika.
Hadi sasa Uhuru ana kura milioni mbili nukta nane
wakati Raila Odinga akiwa na kura milioni mbilii nukta mbili
Raila Odinga alidai kuibiwa ushindi wake mwaka 2007
wakati matokeo yalizua ghasia na kusababisha vifo vya watu zaidi ya laki moja
huku maelfu wakiachwa bila makao
Wakati mamilioni ya wakenya walijitokeza kupiga kura
kwa amani siku ya Jumatatu,watavyopokea matokeo ya mwisho ya kura ndio itakuwa
ishara ya uthabiti wa nchi hiyo.
Ni asilimia arobaini na moja ya kura zilizohesabiwa
huku kukiwa na vituo zaidi ya elfu thelathini ambako kura zilipigiwa.
Ni zaidi ya kura milioni tano zilizohesabiwa kutoka
kwa wapiga kura milioni 14.3 waliokuwa wamesajiliwa.
0 Comment to "MATATIZO YA MITAMBO YA UCHAGUZI KENYA"
Post a Comment