Wafuasi
wa Hugo Chavez wamekuwa wakimuombea aweze kuugua pole
Katika
taarifa kwa taifa, makamu wa rais wa Venezuela Nicholas Marduro ametangaza
kufariki dunia kwa rais Hugo Chavez, 58, kufuatia kuugua muda mrefu maradhi ya
Saratani. Rais Chavez ametoweka katika hadhira ya nchi hiyo kwa muda mrefu
ambapo alikuwa anapokea matibabu nchi jirani ya Cuba.
Alirejea , mjini
Caracas mnamo Februari 18 kwa mara ya kwanza tangu maradhi yake yamzidie ambapo
alipelekwa hospitali ya kijeshi kuendelea kupokea matibau. Hata hivyo maelezo
zaidi hayakutolewa juu ya afya yake. Waandamanaji waliandamana katika mji mkuu
Caracas mwishoni mwa juma wakidai kuwa watu wa Venezuela wanapaswa kupewa
habari zaidi kuhusu afya ya rais wao.
Bwana Chavez amekua
uongozini nchini Venezuela kwa miaka 14 na anatazamiwa kuleta mageuzi makubwa
yaliyolenga zaidi kuimarisha maisha ya raia wa pato la chini.
Ujumbe wa JeshiTaarifa
kutoka kwa jeshi imesema kuwa wataendelea kuilinda hadhi ya nchi na kuimarisha
usalama. Pia jeshi limeahidi kuendelea kuwa waaminifu kwa makamu wa rais Nicholas
Marduro na wakatoa wito kwa raia kuwa watulivu.
CHAVEZ
- WASIFU
Hugo Chavez alijitosa
katika siasa za Venezuela mnamo Februari 1992 akiwa luteni katika jeshi.
Aliongoza mapinduzi dhidi ya rais wa wakati huo Carlos Andres Perez.
Lakini kutokana na
kukosa usaidizi wa kutosha wa kijeshi, Chavez na wanamgambo wenzake walishindwa
kunyakua madaraka hayo. Alikiri kushindwa na aliwekwa korokoroni.
Aliingia uongozini
baada ya ushindi mkubwa ulioviondosha vyama vya kisiasa wakati huo. Katika
kuapishwa kwake mnamo February 1999, Hugo Chavez alitangaza wazi kwamba mipango
yake ya mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi sio kampeni tu. Alitimiza ahadi yake
na kuiongoza nchi hiyo katika mabadiliko ambayo hayakuwahi kushuhudiwa katika
muda wa miongo kadhaa. Alibadili muundo wa bunge na kulifanya kuwa la kikatiba,
ambalo liliiunda katiba mpya baada ya kura ya maoni iliyoidhinishwa na 88% ya
wapiga kura.
Rais Chavez alitaifisha
rasilmali ukiwemo utajiri wake mkubwa wa mafuta. Sera kama hizi zilimfanya
azozane na kampuni za kimataifa za mafuta, lakini alipata uungwaji mkono mkubwa
wa watu maskini.
Kutokana na urafiki
wake na viongozi wa mrengo wa kushoto kama vile rais wa Cuba, Fidel Castro,
ambaye walikuwa na uhusiano wa karibu aligongana kidiplomasia na Marekani,
ambayo ni mshirika wake mkuu wa kibiashara.
Chavez alipendwa
nyumbani na wafuasi wake lakini alipingwa na baadhi ya watu nchini humo na
katika nchi za nje. Alionekana sio tu kama bingwa wa jamii maskini lakini pia
kama muingiliaji wa siasa za nchi jirani. Katika miaka ya hivi karibuni
alilenga kukabiliana na masuala ya ndani ya Venezuela, kama uhalifu, kuinua
uchumi wa nchi na kukabiliana na rushwa.
0 Comment to "RAIS WA VENEZUELA HUGO CHAVEZ AFARIKI"
Post a Comment