Thursday, October 18, 2012

RWANDA INATOA AMRI KWA M23, YASEMA UN

Waziri wa ulinzi nchini Rwanda, ametuhumiwa kwa kuamuru uasi katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa ripoti ya wataalamu wa Umoja wa mataifa.
 Kiongozi wa kisiasa wa M23 Jean Marie Runiga
Ripoti hii inakuja baada ya ripoti nyingine ya Umoja wa Mataifa kutolewa mwezi Juni ambayo ilituhumu Rwanda kwa kuunga mkono waasi hao
Lakini Rwanda na Uganda zimekuwa zikikna madai ya kuunga mkono waasi wa M23.
Duru zinasema kuwa katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, Rwanda imeunga mkono makundi ya waasi Mashariki mwa Congo, kama njia moja ya kupiga vita waasi wa kihutu waliokimbilia eneo hilo baada ya mauaji ya kimbari mwaka 1994.
Baadhi wanatuhumu Rwanda kwa kutumia waasi kupigana vita vyake dhidi ya DRC , nchi ambayo ina utajiri mkubwa wa madini na eneo zima la Maziwa Makuu.
Taarifa za hivi punde za wataalamu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa zinatoa maelezo zaidi kuhusu Rwanda kujihusisha na vita vya DRC.
Wataalamu hao wanasema kuwa waasi wa M23 wanapokea amri za moja kwa moja kutoka kwa mkuu wa majeshi ya Rwanda, Generali Charles Kayonga, " ambaye naye anafuata amri za waziri wa ulinzi Generali James Kabarebe.



Maelfu ya watu wameachwa bila makao kufuatia mapigano Mashariki mwa DRC

Wataalamu hao pia wanasema kuwa Rwanda imekuwa ikitoa silaha kwa waasi hao na kuweka mikakati ya kusajili waasi zaidi ili kuliganya kundi hilo kuwa kubwa.
Maelfu ya watu nchini DRC wamepoteza makao yao kufuatia vita hivyo kati ya waasi na wanajeshi wa Rwanda.
Ripoti hiyo iliyoonwa na shirika la habari la Reuters inasema kuwa wanajeshi wa Rwanda na Uganda wamesaidia waasi wa M23 kupanua harakati zao katika eneo la Mashariki mwa DRC.



Share this

Artikel Terkait

0 Comment to "RWANDA INATOA AMRI KWA M23, YASEMA UN"

Post a Comment