Wachezaji wawili wa Simba, Haruna Moshi Shaaban (Boban) na Juma Said Halfan (Nyoso), wamesimamishwa kuitumikia timu ya wakubwa (senior) kwa sababu na nyakati tofauti.
Moshi amesimamishwa kuichezea timu ya wakubwa kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu na kutokuwa na heshima kwa mwajiri (timu). Klabu imempa Haruna muda wa siku 21 kutoa maelezo kuhusu makosa yake na iwapo atashindwa kutoa maelezo ya kuridhisha, klabu inaweza kumchukulia hatua zaidi.
Katika kipindi hicho (siku 21 kuanzia jana), Boban atapokea nusu ya mshahara wake wa kila mwezi na hatapata marupurupu yoyote yanayohusiana na timu ya wakubwa.
Kwa upande wa Nyoso, uongozi umemwagiza afanye mazoezi na kikosi cha timu ya pili (Simba B) hadi hapo atakapoimarisha kiwango chake cha uchezaji

0 Comment to "SIMBA YAWASIMAMISHA BOBAN NA JUMA NYOSSO"
Post a Comment