Thursday, January 31, 2013

AJALI YA TRENI YAJERUHI WATU 100 AFRIKA KUSINI


 
Magari ya moshi mawili yamegongana nchini Afrika Kusini karibu na mji mkuu wa Pretoria. Takriban watu 100 walijeruhiwa.
Wauguzi walisema kwamba watu 20 walijeruhiwa vibaya katika ajali hiyo.
"Magari moshi yote mawili yalikuwa yamejaa wasafiri ambao husafiri kwenda Pretoria kila siku , wakiwemo watoto wengi tu waliokuwa wanaelekea shuleni,"
Afrika Kusini inakarabati mtandao wake wa safari za gari moshi ambao umezeeka.
Ajali hiyo ilitokea mapema asubuhi jana baada ya gari moshi mmoja lilipogongana na lingine lililokuwa limeegeshwa karibu na Attridgeville, kamji kadogo magharibi mwa Pretoria.

Share this

Artikel Terkait

0 Comment to "AJALI YA TRENI YAJERUHI WATU 100 AFRIKA KUSINI"

Post a Comment